SEHEMU YA 4
Mfalme wa Kwanza wa Israeli Mpaka Utumwa Babeli
Sauli (Saulo) akawa mfalme wa kwanza wa Israeli. Lakini Yehova alimkataa, Daudi akachaguliwa awe mfalme badala yake. Tunajifunza mambo mengi juu ya Daudi. Akiwa kijana, alipigana na jitu Goliathi. Baadaye alimkimbia Mfalme Sauli mwenye wivu. Kisha Abigaili mwenye sura nzuri akamzuia asitende upumbavu.
Halafu, tunajifunza mengi juu ya Sulemani (Solomono), mwana wa Daudi, aliyechukua mahali pa Daudi awe mfalme wa Israeli. Kila mmoja wa wafalme watatu wa kwanza wa Israeli alitawala kwa miaka 40. Baada ya Sulemani kufa, Israeli waligawanyika kuwa falme mbili, ufalme wa kaskazini na wa kusini.
Ufalme wa kaskazini wa makabila 10 uliendelea muda wa miaka 257 kabla ya kuharibiwa na Waashuru. Halafu miaka 133 baadaye, ufalme wa kusini wa makabila mbili ukaharibiwa pia. Wakati huu Waisraeli walihamishwa kupelekwa Babeli. Hivyo Sehemu ya 4 inazungumza historia ya miaka 510, muda ambao mambo mengi ya kusisimua yanatukia mbele yetu.
KATIKA SEHEMU HII
HADITHI 56
Sauli—Mfalme wa Kwanza wa Israeli
Mungu alimchagua na kisha akamkataa, tunaweza kujifunza somo muhimu kutoka kwa Sauli.
HADITHI 58
Daudi na Goliathi
Daudi alimpiga Sauli, si kwa kombeo lake tu bali kwa silaha yenye nguvu zaidi.
HADITHI 59
Sababu Yampasa Daudi Akimbie
Sauli alimpenda Daudi mwanzoni, lakini baadaye alimwonea wivu akataka kumuua. Kwa nini?
HADITHI 60
Abigaili na Daudi
Abigaili asema kwamba mume wake ni mpumbavu, hata hivyo hilo linaokoa uhai wa mume wake kwa muda mfupi.
HADITHI 61
Daudi Anafanywa Mfalme
Daudi anathibitisha kwamba anastahili kuwa mfalme wa Israeli kwa yale anayofanya na anayokataa kufanya.
HADITHI 62
Matata Katika Nyumba ya Daudi
Kwa kosa moja, Daudi anajiletea yeye na familia yake matatizo kwa miaka mingi.
HADITHI YA 64
Sulemani Anajenga Hekalu
Licha ya kuwa na hekima nyingi, Sulemani alishawishiwa kufanya jambo la kipumbavu na lenye kosa.
HADITHI YA 65
Ufalme Unagawanywa
Mara tu Yeroboamu alipoanza kutawala, aliwaongoza watu kuvunja amri za Mungu.
HADITHI YA 67
Yehoshafati Anamtumaini Yehova
Kwa nini jeshi lingeenda kwenye pambano likiwa na waimbaji wasio na silaha wakiongoza njia?
HADITHI YA 68
Wavulana Wawili Wanaokuwa Hai Tena
Je mtu aliyekufa anaweza kuwa hai tena? Imewahi kutokea!
HADITHI YA 69
Msichana Anamsaidia Mwanamume Mwenye Nguvu
Alikuwa na ujasiri wa kusema, na matokeo yake yalikuwa ni muujiza.
HADITHI YA 71
Mungu Anatoa Ahadi ya Paradiso
Paradiso ya kwanza ilikuwa ndogo; paradiso hii itaijaza dunia yote.
HADITHI YA 72
Mungu Anamsaidia Mfalme Hezekia
Katika usiku mmoja, malaika aua wanajeshi 185,000 wa Ashuru.
HADITHI YA 74
Mwanamume Asiyeogopa
Yeremia alifikiri alikuwa mdogo sana kuwa nabii, lakini Mungu alijua kwamba angeweza kuwa nabii.
HADITHI YA 76
Yerusalemu Unaharibiwa
Kwa nini Mungu aliwaruhusu maadui wa Israeli, Wababeli, waharibu Yerusalemu?