Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

HADITHI YA 68

Wavulana Wawili Wanaokuwa Hai Tena

Wavulana Wawili Wanaokuwa Hai Tena

KAMA ungekufa, mama yako angeonaje ukiwa hai tena? Angefurahi sana! Je! imepata kutokea hivyo zamani?

Mwanamume huyu ni nabii Eliya. Mwanamke ni mjane wa mji wa Zarefati, na mvulana ni mwanawe. Basi, siku moja mvulana anakuwa mgonjwa sana mpaka mwishowe anakufa.

Eliya anamchukua mtoto aliyekufa kwenye orofa na kumlaza kitandani. Ndipo anasali hivi: ‘Ee Yehova, acha mtoto huyu awe hai tena.’ Mtoto aanza kupumua! Kisha Eliya amrudisha chini na kumwambia mwanamke: ‘Tazama, mwanao yuko hai!’ Ndiyo sababu mama huyo anafurahi sana.

Nabii mwingine wa maana wa Yehova ni Elisha. Anamsaidia Eliya. Lakini wakati fulani Yehova anamtumia Elisha pia afanye miujiza. Siku moja Elisha anakwenda kwenye mji wa Shunemu, ambako mwanamke mmoja anamkaribisha vizuri. Baadaye mwanamke huyo anazaa mtoto wa kiume.

Asubuhi moja, mtoto huyo akiisha kuwa mkubwa kidogo, anakwenda kufanya kazi shambani pamoja na babaye. Mara moja mvulana huyo anapaza sauti: ‘Naumwa kichwa!’ Baada ya kupelekwa nyumbani, anakufa. Lo! mama yake anahuzunika! Mara hiyo mama anakwenda kumwita Elisha.

Elisha anapofika, anaingia chumbani akiwa na mtoto aliyekufa. Anamwomba Yehova, na kulalia mwili wake. Upesi mwili wa mtoto wapata moto, anapiga chafya mara saba. Mama yake anapoingia na kuona mtoto wake yuko hai, anafurahi wee!

Watu wengi wamekufa. Jamaa na rafiki zao wamehuzunishwa sana na hilo. Sisi hatuwezi kufufua wafu. Yehova anaweza. Baadaye tutajifunza atakavyofufua mamilioni ya watu.