Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

SEHEMU YA 5

Utumwa Babeli Mpaka Kujengwa Upya Kuta za Yerusalemu

Utumwa Babeli Mpaka Kujengwa Upya Kuta za Yerusalemu

Wakiwa utumwani Babeli, imani ya Waisraeli ilijaribiwa sana. Shadraka, Meshaki na Abedʹne·go walitupwa katika tanuru (jiko) ya moto mkali, lakini Mungu akawaokoa. Baadaye, Babeli ukiisha kushindwa na Wamedi na Waajemi, Danieli alitupwa katika shimo la simba, lakini Mungu alimlinda pia kwa kuvifunga vinywa vya simba.

Mwishowe, Koreshi mfalme wa Ajemi akawakomboa Waisraeli. Walirudi kwao ilipotimia miaka 70 baada ya kupelekwa Babeli kama mateka. Jambo la kwanza walilofanya waliporudi Yerusalemu ni kujenga hekalu la Yehova. Lakini, upesi adui wakazuia kazi yao. Hivyo walimaliza kujenga hekalu kwa muda wa karibu miaka 22 baada ya kurudi Yerusalemu.

Halafu, tunajifunza habari ya safari ya Ezra akirudi Yerusalemu akalipambe hekalu. Hiyo ilikuwa miaka 47 baada ya kumaliza kujenga hekalu. Kisha, miaka 13 baada ya safari ya Ezra, Nehemia alisaidia kujenga upya kuta za Yerusalemu zilizobomoka. Sehemu ya 5 inazungumza historia ya miaka 152 kufikia wakati huo.

 

KATIKA SEHEMU HII

HADITHI YA 77

Walikataa Kuabudu

Je, Mungu atawaokoa vijana hawa watatu waliomtii kutoka katika tanuru ya moto?

HADITHI YA 78

Mwandiko wa Mkono Ukutani

Nabii Danieli akifafafanua maneno manne ya kifumbo.

HADITHI YA 79

Danieli Katika Shimo la Simba

Danieli alihukumiwa adhabu ya kifo, lakini je, angeweza kuiepuka?

HADITHI YA 80

Watu wa Mungu Wanatoka Babeli

Mfalme Koreshi wa Uajemi alitimiza unabii mmoja alipoteka Babiloni, na sasa anatimiza unabii mwingine.

HADITHI YA 81

Kuutumainia Msaada wa Mungu

Waisraeli wavunja amri za wanadamu ili kumtii Mungu. Je Mungu atawabariki?

HADITHI YA 82

Mordekai na Esta

Malkia Vashti alikuwa mrembo, lakini Mfalme Ahasuero alimchagua Esta kama malkia wake mpya. Kwa nini?

HADITHI YA 83

Kuta za Yerusalemu

Wakijenga upya kuta, wafanya-kazi walipaswa kuweka panga na mikuki yao tayari usiku na mchana.