SEHEMU YA 6
Kuzaliwa Yesu Mpaka Kufa Kwake
Malaika Gabrieli alitumwa kwa msichana mzuri jina lake Mariamu (Maria). Akamwambia ya kuwa angezaa mtoto ambaye angetawala milele akiwa mfalme. Mtoto huyo, Yesu, alizaliwa katika boma la ng’ombe, ambamo wachungaji walimtembelea. Baadaye, nyota ikaongoza watu kutoka Mashariki mpaka kwenye mtoto mchanga. Twajifunza aliyeonyesha nyota hiyo, na namna Yesu alivyookolewa asiuawe.
Halafu, Yesu akiwa mwenye miaka 12, twamwona akizungumza na waalimu katika hekalu. Miaka kumi na minane baadaye Yesu anabatizwa, kisha aanza kazi ya kuhubiri Ufalme na kufundisha ambayo Mungu alimtuma duniani aifanye. Ili wamsaidie kazi hiyo, Yesu alichagua wanaume 12 akawafanya mitume wake.
Pia Yesu alifanya miujiza mingi. Alilisha maelfu ya watu samaki wachache na mikate michache. Aliponya wagonjwa na hata kufufua wafu. Mwishowe, twajifunza mambo mengi yaliyompata Yesu siku ya mwisho ya kuishi kwake, na namna alivyouawa. Yesu alihubiri muda wa miaka mitatu na nusu, basi Sehemu ya 6 inazungumza kipindi cha miaka mingi kidogo kuliko 34.
KATIKA SEHEMU HII
HADITHI YA 84
Malaika Anatembelea Mariamu
Analeta ujumbe kutoka kwa Mungu: Mariamu atapata mtoto ambaye atakuwa mfalme milele.
HADITHI YA 85
Yesu Anazaliwa Katika Boma la Ng’ombe
Kwa nini mfalme anayekuja azaliwe mahali ambapo wanyama wanalishiwa?
HADITHI YA 86
Wanaume Walioongozwa na Nyota
Ni nani aliyewaongoza mamajusi kwa Yesu? Jibu linaweza kukushangaza.
HADITHI YA 87
Kijana Yesu Katika Hekalu
Ana mambo ambayo yanawashangaza hata watu wazima wanaofundisha katika hekalu.
HADITHI YA 88
Yohana Anambatiza Yesu
Yohana amekuwa akiwabatiza watenda dhambi, lakini Yesu hajatenda dhambi kamwe. Kwa nini Yohana alimbatiza?
HADITHI YA 89
Yesu Anasafisha Hekalu
Yesu anaonyesha aina ya upendo ambao unamsukuma kuwa na hasira.
HADITHI YA 90
Pamoja na Mwanamke Penye Kisima
Maji ambayo Yesu atampa yatawezaje kumfanya asione kiu tena kamwe?
HADITHI YA 91
Yesu Anafundisha Juu ya Mlima
|Jifunze hekima isiyopitwa na wakati kutoka katika Mahubiri ya Mlimani ya Yesu.
HADITHI YA 92
Yesu Anafufua Wafu
Kwa kutumia nguvu za Mungu, Yesu alisema maneno mawili rahisi na kumfufua binti ya Yairo.
HADITHI YA 93
Yesu Analisha Watu Wengi Chakula
Kwa kuwalisha maelfu ya watu kimuujiza, Yesu alithibitisha jambo gani muhimu?
HADITHI YA 94
Anapenda Watoto Wadogo
Yesu aliwafundisha mitume kwamba wana mengi ya kujifunza si tu kuhusu watoto wadogo bali pia kutoka kwa watoto wadogo.
HADITHI YA 95
Namna Yesu Anavyofundisha
Mfano wa Yesu wa jirani Msamaria ni mmoja kati ya mifano mingi inayoonyesha njia yake ya kufundisha aliyoitumia kwa ukawaida.
HADITHI YA 97
Yesu Aja Kama Mfalme
Umati mkubwa unamkaribisha Yesu, lakini si wote wanaofurahishwa na jambo hilo.
HADITHI YA 98
Juu ya Mlima wa Mizeituni
Yesu aliwaambia mitume wake wanne mambo ambayo yanatukia katika siku zetu.
HADITHI YA 99
Katika Chumba cha Juu
Kwa nini Yesu anawaambia mitume wake waadhimishe mlo huu wa pekee kila mwaka?
HADITHI YA 101
Yesu Anauawa
Akiwa ametundikwa juu ya mti wa mateso, Yesu alitoa ahadi kuhusu paradiso.