Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

SANDUKU LA KUFUNDISHIA LA 2B

Ezekieli​—Maisha na Nyakati Zake

Ezekieli​—Maisha na Nyakati Zake

Jina Ezekieli linamaanisha “Mungu Huimarisha.” Ingawa unabii anaotoa una maonyo mengi, ujumbe wake kwa ujumla unapatana na maana ya jina lake na unaimarisha imani ya watu wanaotaka kumtolea Mungu ibada safi.

MANABII WA NYAKATI ZAKE

  • YEREMIA,

    alitoka katika familia ya kikuhani, alitumikia hasa Yerusalemu (647 hadi 580 K.W.K)

  • HULDA

    alitumikia wakati kitabu cha Sheria kilipopatikana hekaluni karibu mwaka wa 642 K.W.K.

  • DANIELI,

    alitoka katika kabila la kifalme la Yuda, alipelekwa Babiloni mwaka wa 617 K.W.K.

  • HABAKUKI

    huenda alitumikia Yuda mwanzoni mwa utawala wa Yehoyakimu

  • OBADIA

    alitoa unabii dhidi ya Edomu, huenda wakati wa kuharibiwa kwa Yerusalemu

WALITABIRI LINI? (TAREHE ZOTE NI K.W.K.)

MATUKIO MUHIMU KATIKA MAISHA YA EZEKIELI (TAREHE ZOTE NI K.W.K.)

  1. Karibu 643: Azaliwa

  2. 617: Achukuliwa mateka kwenda Babiloni

  3. 613: Aanza kutabiri; aona maono ya Yehova

  4. 612: Aona maono ya uasi hekaluni

  5. 611: Aanza kushutumu Yerusalemu

  6. 609: Mke wake afa na Yerusalemu laanza kuzingirwa kwa mara ya mwisho

  7. 607: Apokea uhakikisho kwamba Yerusalemu limeharibiwa

  8. 593: Aona maono ya hekalu

  9. 591: Atabiri kwamba Nebukadneza atavamia Misri; akamilisha maandishi yake

WAFALME WA YUDA NA BABILONI

  1. 659-629: Yosia atetea ibada safi lakini anakufa vitani akipigana na Farao Neko

  2. 628: Yehoahazi atawala vibaya kwa miezi mitatu naye atekwa na Farao Neko

  3. 628-618: Yehoyakimu ni mfalme mbaya na Farao Neko anamfanya kuwa kibaraka

  4. 625: Nebukadneza ashinda jeshi la Wamisri

  5. 620: Nebukadneza avamia Yuda kwa mara ya kwanza na kumfanya Yehoyakimu kuwa kibaraka wake huko Yerusalemu

  6. 618: Yehoyakimu amwasi Nebukadneza lakini huenda anakufa Wababiloni wanapovamia Nchi ya Ahadi kwa mara ya pili.

  7. 617: Yehoyakini, anayeitwa pia Yekonia, ni mfalme mbaya anayetawala kwa miezi mitatu, kisha anajisalimisha kwa Nebukadneza

  8. 617-607: Mfalme mwovu na mwoga Sedekia, afanywa kuwa kibaraka na Nebukadneza

  9. 609: Sedekia anamwasi Nebukadneza, ambaye anavamia tena Yuda kwa mara ya tatu

  10. 607: Nebukadneza aharibu Yerusalemu, amkamata Sedekia, ampofusha, na kumpeleka Babiloni