Hamia kwenye habari

Matembezi ya Betheli

Tunakualika kwa uchangamfu utembelee ofisi zetu za tawi, tunazoziita Betheli. Baadhi ya ofisi zetu zina maonyesho utakayotembelea ukiwa peke yako.

Kurejea kwa Matembezi ya Ofisi: Katika nchi nyingi, tutaanza tena kuruhusu matembezi katika ofisi zetu za tawi kuanzia Juni 1, 2023. Ili kupata habari zaidi, wasiliana na ofisi ya tawi unayopenda kuitembelea. Tafadhali usitembelee ofisi ya tawi ikiwa una ugonjwa wa Virusi vya Corona (COVID-19), una dalili za homa au mafua, au hivi karibuni ulishirikiana na mtu aliye na ugonjwa wa COVID-19.

Brazili

Habari Kuhusu Matembezi

Toa ombi la Matembezi

Angalia au Ubadili Maombi

Pakua Broshua ya Matembezi

Maonyesho

Biblia—Kitabu na Mtungaji wa Biblia. Maonyesho haya yanampa utukufu anaostahili Mwandishi wa Biblia, yaani, Yehova Mungu na pia yamekazia ujumbe mkuu wa Biblia: Ufalme wa Mungu. Wageni watapendezwa kuona jinsi Biblia ilivyookoka kufikia siku zetu, wakati huohuo ujumbe wake haujabadilishwa licha ya jitihada nyingi za wapinzani waliojaribu kuibadilisha.

Maonyesho ya Kihistoria. Maonyesho haya yanayonyesha jinsi Yehova alivyobariki kazi ya kuhubiri Ufalme wake nchini Brazili kwa zaidi ya miaka 120. Wageni watakaotembelea wataweza kuona utafiti wa kihistoria unaonyesha habari mpya zilizopatikana hivi karibuni kuhusu jinsi kazi ya kuhubiri ilivyoanza na kukua nchini Brazili licha ya upinzani na mateso waliyokabili.

Anwani na Namba ya Simu

Omba Maelekezo