Mashahidi wa Yehova—Taarifa Fupi Kulingana na Nchi

Urusi

TAARIFA ZA HABARI

Wamefungwa kwa Sababu ya Imani Yao​—Urusi

Mashahidi wa Yehova nchini Urusi wamefungwa gerezani kwa sababu ya imani yao. Jifunze historia yao na upate orodha unayoweza kuchapisha ya Mashahidi wowote walio gerezani wakati huu.

Urusi Yashambulia Ukrainia​—Je, Unabii wa Biblia Unatimizwa?

Ikiwa ndivyo, je, Biblia inafunua jinsi mambo yote haya yatakavyokwisha?

TAARIFA ZA HABARI

Mashahidi wa Yehova Wanamuunga Mkono Ndugu Konstantin Bazhenov Wakati wa Kifungo Chake, Kuachiliwa, na Kufukuzwa Nchini

Konstantin Bazhenov ni mmoja kati ya Mashahidi wa Yehova nchini Urusi kukamilisha kifungo chake tangu marufuku iliyotangazwa na Mahakama Kuu mwaka wa 2017. Mei 5, 2021, baada ya kuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu, aliachiliwa mapema na muda mfupi baada ya hapo akafukuzwa nchini.

TAARIFA ZA HABARI

Mashahidi wa Yehova Katika Eneo la Irkutsk Wadumisha Uaminifu Licha ya Kuvamiwa kwa Ukatili Nyumbani

Oktoba 4, 2021, mfululizo wa uvamizi wa nyumba ulitukia katika eneo la Irkutsk. Wakati wa uvamizi huo Mashahidi wahojiwa na kupigwa kwa ukatili. Baada ya hapo, Mashahidi sita wa Yehova walipelekwa mahabusu kwa sababu tu ya kushiriki imani yao ya Kikristo kwa amani.

TAARIFA ZA HABARI

Urusi Yaitangaza Biblia Kuwa na “Msimamo Mkali”

Mahakama ya Jiji la Vyborg iliitangaza Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ya lugha ya Kirusi kuwa na ‘msimamo mkali,’ Biblia hiyo inachapishwa na Mashahidi wa Yehova katika lugha nyingi.

Ona Pia