Hamia kwenye habari

Awamu ya 1 ya Picha za Wallkill (Julai 2013 Hadi Oktoba 2014)

Awamu ya 1 ya Picha za Wallkill (Julai 2013 Hadi Oktoba 2014)

Mashahidi wa Yehova wanapanua na kuboresha majengo yao yaliyoko Wallkill, New York. Picha hizi zinaonyesha baadhi ya kazi zilizofanywa kati ya Julai 2013 na Oktoba 2014. Mradi huo umeratibiwa kukamilika Novemba 2015.

Picha ya majengo ya Wallkill kufikia Oktoba 21, 2013.

  1. Kinu (kiliondolewa Januari 2014)

  2. Dobi ya ziada

  3. Chumba cha kulia chakula

  4. Makazi E

  5. Jengo la Huduma

  6. Kiwanda cha Kuchapishia

  7. Shawangunk Kill (kijito)

Julai 12, 2013​—Dobi ya ziada

Kreni likiinua na kusimamisha kuta. Kuta hizo ziliunganishiwa katika eneo la ujenzi.

Julai 19, 2013​—Makazi E

Wafanyakazi wakiweka ukanda wa plastiki unaotumiwa kusaidia jengo kuhimili matetemeko ya ardhi (Fiber Reinforced Polymer) katika sakafu ya saruji (Dox Plank). Mita 7,600 hivi za FRP zilitumiwa katika jengo lote.

Agosti 5, 2013​—Makazi E

Upande wa nje wa ukuta wa matofali ukirekebishwa.

Agosti 30, 2013​—Dobi ya ziada

Fremu za chuma zinawekwa kwa ajili ya chumba cha kuhifadhia vifaa vya ufundi.

Septemba 17, 2013​—Makazi E

Mfanyakazi akikata mkeka mwepesi ambao umewekwa juu ya paa.

Oktoba 15, 2013​—Makazi E

Wafanyakazi wakihakikisha hakuna nafasi zilizobaki chini ya ukanda wa FRP. Nafasi zikipatikana, plastiki zaidi huongezwa.

Novemba 15, 2013​—Dobi ya ziada

Baadhi ya kazi zinazofanywa juu ya paa zinatia ndani kuweka mfumo wa kupitisha hewa.

Desemba 9, 2013​—Makazi E

Gundi ya kushikilia jengo ikiwekwa kwenye nyufa ndani ya saruji ya paa. Kazi ya kuimarisha jengo dhidi ya matetemeko ya ardhi ilichukua mwaka mmoja na nusu hivi.

Desemba 11, 2013​—Dobi ya ziada

Mfanyakazi akitengeneza mahali pa kuweka bomba la kupitishia maji-taka.

Januari 10, 2014​—Kinu

Ghala la nafaka linaloonekana likiondolewa lilitumika tangu miaka ya 1960 hadi 2008 hivi. Liliacha kutumika kuku, ng’ombe, na nguruwe walipoacha kufugwa Wallkill.

Januari 22, 2014​—Jengo la Huduma

Viti vikiondolewa ili kukarabati upya ukumbi.

Januari 29, 2014​—Kinu

Maghala haya ya nafaka yalitumiwa kuhifadhi chakula cha mifugo.

Machi 3, 2014​—Kiwanda cha Uchapishaji

Majengo mapya ya Idara ya Mazoezi ya Ufundi yakijengwa.

Julai 4, 2014​—Jengo la Huduma

Mtia weko akiimarisha nguzo ya jengo.

Septemba 19, 2014​—Chumba cha kulia chakula (Makazi E)

Zulia likiwekwa kwenye chumba kilichotumiwa na wajenzi kulia chakula.

Septemba 22, 2014​—Makazi E

Kumalizia kujenga ukuta kwenye orofa ya kwanza.

Septemba 24, 2014​—Jengo la Huduma

Vyuma vinawekwa kwa ajili ya lifti mpya ya jengo.

Oktoba 2, 2014​—Chumba cha kulia chakula (Makazi E)

Chumba cha kulia chakula kimepanuliwa ili kiweze kutoshea watu 1,980.

Oktoba 22, 2014​—Jengo la Huduma

Kupanua eneo lililo karibu na nguzo ili kuongezea upana wake. Hilo litasaidia jengo liwe na uwezo wa kuhimili matetemeko ya ardhi.