Hamia kwenye habari

Awamu ya 2 ya Picha za Warwick (Septemba Hadi Desemba 2014)

Awamu ya 2 ya Picha za Warwick (Septemba Hadi Desemba 2014)

Katika picha hizi, utaona maendeleo ya ujenzi yaliyofanywa kwenye makao makuu ya Mashahidi wa Yehova kati ya mwezi wa Septemba na Desemba 2014.

Picha ya eneo lote la ujenzi la Warwick litakapokamilika. Kuanzia kushoto juu kwenda kulia:

  1. Jengo la Gereji

  2. Jengo la Maegesho ya Magari ya Wageni

  3. Jengo la Udumishaji na Maegesho ya Wenyeji

  4. Jengo la Makazi B

  5. Jengo la Makazi D

  6. Jengo la Makazi C

  7. Jengo la Makazi A

  8. Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Septemba 11, 2014​—Maegesho ya Wageni

Kuunganisha mihimili ya chuma ya paa la jengo la makazi C.

Septemba 18, 2014​—Eneo la ujenzi la Warwick

Picha iliyopigwa upande wa kusini mwa eneo la ujenzi, ikionyesha upande wa kaskazini wenye Ziwa la Sterling Forest (Ziwa la Blue Lake). Kreni 13 hivi zimekuwa zikifanya kazi kwa wakati mmoja katika ujenzi huu. Upande wa mbele wa picha, zege inamwagwa kwenye msingi wa jengo la makazi B.

Septemba 26, 2014​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Maboriti na nguzo za chuma zikiwa tayari kutumiwa. Ujenzi huo wa kutumia chuma katika jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali, unafanya iwe rahisi kujenga vyumba vyenye eneo kubwa la sakafu na pia kuongeza kasi ya ujenzi.

Oktoba 9, 2014​—Eneo la ujenzi la Warwick

Wajenzi wakiunganisha mihimili ya paa iliyofunikwa kwa mabati na mkeka wa kuzuia maji kwa ajili ya paa la jengo la makazi C. Upande wa nyuma na kushoto, paa jingine linaendelea kuunganishwa.

Oktoba 15, 2014​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Wajenzi wanasimamisha maboriti ya chuma upande wa kusini-magharibi mwa jengo. Upande huu wa jengo utakuwa na jiko, chumba cha kulia, dobi, na idara nyingine za kutoa utegemezo.

Oktoba 15, 2014​—Eneo la ujenzi la Warwick

Fundi-bomba akipewa ufagio.

Oktoba 20, 2014​—Eneo la ujenzi la Warwick

Ukuta huu wa mfano ulisaidia wajenzi kuamua mbinu za ujenzi, rangi ya saruji itakayotumiwa, na njia mbalimbali za kuunganisha matofali. Ulitumiwa pia kuwazoeza wajenzi wapya waliokuwa wakiwasili. Kwenye picha, ukuta huo unabomolewa baada ya kutimiza kusudi lake.

Oktoba 31, 2014​—Jengo la Makazi C

Kipande cha paa lililounganishwa awali kikiwekwa mahali pake. Kuta zilizo sehemu ya paa zenye umbo la pembe tatu zinasaidia kurembesha mwonekano wa paa unapolitazama jengo kutoka mbali.

Novemba 7, 2014​—Jengo la Udumishaji na Maegesho ya Wenyeji

Tangi la mafuta lenye uwezo wa kubeba lita 95,000 linawekwa mahali pake. Matangi haya yatabeba mafuta ya kuchemshia maji.

Novemba 12, 2014​—Jengo la Makazi C

Picha ya upande wa kusini mwa jengo, na Ziwa la Blue Lake linaonekana upande wa kulia wa picha. Rangi na aina mbalimbali za kutia nakshi zinatumiwa ili kurembesha mwonekano wa majengo.

Novemba 21, 2014​—Jengo la Udumishaji na Maegesho ya Wenyeji

Wenzi wa ndoa walio kwenye kikosi cha mafundi-bomba wanaweka mifereji/mabomba ya kupitisha maji kabla ya sakafu ya jengo kuwekwa.

Novemba 28, 2014​—Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali

Kuondoa theluji juu ya paa.

Desemba 1, 2014​—Jengo la Udumishaji na Maegesho ya Wenyeji

Wenzi wa ndoa wengine wakipitia michoro ya mfumo wa kupitisha maji.

Desemba 10, 2014​—Jengo la Udumishaji na Maegesho ya Wenyeji

Kuchimba, kuweka mbao za kushikilia zege, na kumwagwa kwa zege kunaendelea hata katika siku yenye theluji. Upande wa juu kushoto wa picha, sehemu fulani za Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali zimefunikwa kwa plastiki ili kazi zinazoathiriwa na hali ya hewa, kama vile kukamilisha sakafu na kuweka mfumo wa kuzuia moto, ziendelee hata wakati wa baridi kali.

Desemba 12, 2014​—Jengo la Makazi D

Wajenzi wakiweka mkeka wa kuzuia unyevunyevu kwenye nguzo na kwenye ncha za sakafu kabla ya ukuta kuwekwa.

Desemba 15, 2014​—Eneo la ujenzi la Warwick

Picha iliyopigwa kutoka angani ikionyesha upande wa magharibi. Majengo ya makazi yako upande wa juu wa picha. Jengo kubwa jeupe linaloonekana katikati ya picha ni Jengo la Ofisi na Huduma Mbalimbali. Eneo la ujenzi ni chini ya asilimia 20 ya ekari 100 hivi za eneo lote lililonunuliwa. Eneo linalosalia limebaki kuwa msitu.

Desemba 15, 2014​—Eneo la ujenzi la Warwick

Picha iliyopigwa kutoka angani ikionyesha upande wa mashariki, wenye majengo ya makazi C na D karibu upande wa chini wa picha. Kwenye jengo la makazi C, wajenzi wanamalizia kuweka paa.

Desemba 25, 2014​—Jengo la Makazi C

Fundi-seremala akimalizia kuweka sakafu kwenye chumba cha mfano. Mbinu nne mbalimbali zilizochaguliwa mapema zitatumiwa kumalizia vyumba vya makazi. Mbinu hizo zinatia ndani aina ya rangi, zulia, sakafu, vigae vya sakafu, na meza.

Desemba 31, 2014​—Majengo ya Ofisi na Huduma Mbalimbali

Kusawazisha sakafu ya saruji kwa mkono kwa njia ambayo maji yataweza kutiririka.

Desemba 31, 2014​—Jengo la Makazi C

Fundi-umeme mwenye umri wa miaka 77 akipitisha nyaya za mawasiliano. Kufikia mwisho wa mradi huu wa ujenzi, kilomita 32 hivi za nyaya hizo zitakuwa zimetumika.