Awamu ya 2 ya Picha za Uingereza (Septemba 2015 hadi Agosti 2016)
Mashahidi wa Yehova nchini Uingereza wanahamisha ofisi ya tawi kutoka Mill Hill, London, hadi eneo lililo kilomita 70 hivi mashariki, karibu na jiji la Chelmsford, Essex. Katika picha hii, tutaona jinsi kazi inavyoendelea katika ofisi mpya ya tawi kati ya Septemba 2015 na Agosti 2016.
Oktoba 29, 2015—Eneo la kutegemeza ujenzi
Wafanyakazi wamwaga saruji mbele ya gereji itakayotumiwa kuweka mashine za ujenzi.
Desemba 9, 2015—Eneo la kutegemeza ujenzi
Wajenzi wakiweka paa juu ya jengo litakalokuwa na ofisi na chumba cha kulia chakula wakati wa ujenzi.
Januari 18, 2016—Eneo la kutegemeza ujenzi
Kwenye mwingilio mkuu, mjenzi anatumia gari yenye msumeno ili kukata miti kadhaa. Gari hilo lina kitu kinachobana mti na kukata shina, kisha kuuondoa mti huo. Kwa sababu wanakata miti kadhaa, watapanda miti mingi sana kabla ya kumaliza mradi huo.
Machi 31, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Wajenzi waondoa vitu visivyotakiwa kwenye udongo ambavyo viliachwa na mmiliki aliyetangulia wa eneo hilo. Baada ya hapo, udongo unaweza kusafishwa na kutumiwa tena.
Aprili 14, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Wafanyakazi watayarisha kubeba vyumba vya muda wakitumia kreni. Kikosi cha ujenzi na wanakandarasi watatumia vyumba hivyo kama ofisi.
Mei 5, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Wafanyakazi watenganisha vitu vilivyopo ili vitumiwe tena. Halmashauri ya Mradi wa Ujenzi ilikuwa na lengo la kugeuza takataka zisizo hatari zisiingie kwenye mashimo waliyochimbua, nao wamefaulu kufikia lengo hilo. Isitoshe, asilimia 89 ya vifusi vya majengo yaliyoharibiwa—kama vile matofali, saruji, na mbao,—vimetumika tena katika ujenzi.
Mei 23, 2016—Eneo la kutegemeza ujenzi
Mjenzi akijaza mchanga kwenye mtaro. Eneo hilo litatumiwa kwa ajili ya makao ya muda ya wajenzi.
Mei 26, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Mwanakandarasi akikusanya sampuli za udongo ili kuzipima kujua ikiwa zinafaa kujenga barabara katika eneo hilo.
Mei 31, 2016—Ofisi ya tawi itakavyoonekana
Mei 31, 2016, Baraza Linaloongoza liliidhinisha michoro hii. Baada ya kupokea idhini hiyo, pamoja na idhini kutoka kwa wenye mamlaka wa eneo hilo, sasa mradi wa ujenzi unaweza kuanza.
Juni 16, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Wafanyakazi wakitoa vitu visivyohitajiwa kutoka kwenye udongo uliochimbuliwa katika eneo hilo. Kisha udongo huo unaweza kutumiwa sehemu nyingine. Kazi hiyo inapunguza gharama za kutolewa udongo kwenye eneo hilo na kununua udongo mwingine wa kujaza eneo hilo.
Juni 20, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Wafanyakazi waondoa udongo kwenye eneo ambalo barabara itajengwa. Kazi hiyo iliendelea licha ya mvua kubwa iliyonyesha kwa mwezi mzima, ambayo ilifanya sehemu fulani iwe na matope mengi.
Julai 18, 2016—Eneo la kutegemeza ujenzi
Barabara zinanyunyiziwa maji ili kupunguza vumbi. Kazi ya kudumisha eneo la ujenzi katika hali ya kupendeza ni sehemu ya kazi ya shirika la Considerate Constructors Scheme, ambalo Halmashauri ya Mradi wa Ujenzi imejiandikisha ili kuhakikisha wanafuata sheria za eneo hilo zinazohusu ujenzi. Mazoea yanayopendekezwa na shirika hilo yanapatana na viwango vya Biblia kwa kupendekeza kwamba watu waheshimu jamii na kuwajali majirani.
Julai 18, 2016—Eneo la kutegemeza ujenzi
Mkata-vyuma akata vyuma ambavyo vitafungiwa mabomba ya viyoyozi.
Julai 22, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Wafanyakazi wakitenganisha mchanga uliochanganyika na vifusi wenye ukubwa wa mita 20,000 za mraba. Kama unavyoona sehemu ya kati ya picha, mchanga unaingizwa kwenye gari fulani. Likitumia vichujio vya ukubwa tofauti-tofauti, uchafu unatenganishwa na mchanga uliochujwa unatokea sehemu ya chini. Mitambo mitatu inasafirisha uchafu kwenye lori kadhaa.
Julai 22, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Wanakandarasi wahamisha udongo mwingi sana ili sehemu ya chini ya eneo hilo ilingane na matakwa ya miradi ya ujenzi.
Agosti 18, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Sehemu ya kati upande wa kushoto wa picha, wanakandarasi wamemaliza kusawazisha udongo ili msingi wa majengo ya makazi uanze kuchimbwa. Kushoto zaidi kuna sehemu iliyokamilika ya makazi ya muda, wajenzi 118 wanaweza kuishi hapo.