Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW BROADCASTING

Chagua Video Kupitia Apple TV

Chagua Video Kupitia Apple TV

Unaweza kucheza, kutua, kupeleka mbele, kurudisha nyuma, na kuruka unapotazama video. Tazama video moja au video zote zilizopo.

(Taarifa: Mwonekano wa kifaa cha kubadili vipindi unaoonyeshwa kwenye miongozo hii unaweza usifanane na kifaa chako.)

 Tafuta na Tazama Video

Chagua sehemu ya Video iliyo mwanzoni mwa kurasa ili kuona video zilizopo katika sehemu hiyo.

Tumia kifaa chako (Siri Remote) kuchagua vipengele. Kipengele utakachochagua kitakuwa na picha kubwa kuliko vingine.

  • Tumia kifaa chako (Siri Remote) kuchagua vipengele. Kipengele utakachochagua kitakuwa na picha kubwa kuliko vingine.

  • Bonyeza kipengele ulichochagua.

Baadhi ya video zinapatikana katika vipengele mbalimbali. Kwa mfano, video ya Mwana Mpotevu Arudi, inapatikana kwenye kipengele cha Sinema, Familia na Vijana.

Chagua neno Changanya ili kucheza video zote katika kipengele kimoja kwa mfululizo bila kuzingatia mpangilio ulio kwenye orodha.

Kila kipengele kina mkusanyiko wa video. Jina la kipengele litaonekana juu ya kipengele hicho.

  • Telezesha Juu au Chini ili kupata mkusanyo mwingine.

  • Telezesha Kushoto au Kulia ili kupata video utakayo kwenye mkusanyo.

Kuna njia mbili za kutazama video katika mkusanyo:

  • Kila mkusanyiko wa video una sehemu ya Cheza Zote. Unaweza kuchagua cheza zote ili utazame video zote katika mkusanyiko ukianzia video ya kwanza.

  • Chagua neno Changanya ili kucheza video zote katika kipengele kimoja kwa mfululizo unaofuatana au usiofuatana.

Taarifa: Video zilizopo zikiisha itaacha kucheza.

Chagua video ili kuona Maelezo ya Video.

Chagua video ili kuona sehemu ya Maelezo ya Video.

Chagua mojawapo ya mambo haya:

  • Cheza: Cheza video kutoka mwanzo.

  • Cheza Zote: Cheza video zote kwenye mkusanyo huu, kuanzia video inayoonekana kwenye skrini. Video zinapomaliza kuchezwa kwenye mkusanyo huu zitaacha kucheza.

  •   Anza Tena: Anza tena video kutoka mahali ulipoishia kutazama.

Kipengele chini ya sehemu ya Maelezo ya Video inaonyesha mikusanyo mingine ya video inayoonekana kwenye skrini. Bonyeza Chini ili kuingia kwenye kipengele hicho, na Juu ili kurudi kwenye sehemu ya Maelezo ya Video.

Tua, Peleka mbele, Rudisha nyuma video

Unapotazama video, unaweza kutumia kifaa cha kubadili kipindi cha Siri (Siri Remote) kama ifuatavyo:

  • Cheza/Tua: Simamisha kwa muda video. Bonyeza kitufe hicho hicho kuanza tena. Pia unaweza kubonyeza sehemu ya kati ya kibonyezo ili kucheza au kusimamisha kwa muda.

  • Rudisha Nyuma: Telezesha upande wa Kushoto wakati umesimamisha kwa muda video ili kurudi mpaka mwanzo wa video. Bonyeza kitufe cha Cheza/Tua ili kuendelea kucheza.

  • Peleka Mbele: Telezesha upande wa Kulia wakati umesimamisha kwa muda video ili kupeleka mbele video. Bonyeza kitufe cha Cheza/Tua ili kuendelea kucheza.

  • Hatua Mbele: Ili kurusha video mbele kwa sekunde kumi, weka kidole chako kwenye upande wa kulia wa sehemu ya kutelezesha ya kibonyezo chako.

  • Unapoona alama ya Kurusha imetokea kwenye sehemu ya chini ya skrini, bonyeza sehemu ya Kutelezesha.

  • Hatua Nyuma: Ili kurusha video nyuma kwa sekunde kumi, weka kidole chako kwenye upande wa kushoto wa sehemu ya kutelezesha ya kibonyezo chako.

  •  Unapoona alama ya Kurusha imetokea kwenye sehemu ya chini ya skrini, bonyeza sehemu ya Kutelezesha.

  • Menyu: Rudi kwenye sehemu ya Maelezo ya Video.

Tazama Video za Karibuni au Zilizoteuliwa

Ukurasa wa mwanzo wa JW Broadcasting una orodha mbili za pekee za mkusanyo wa Chagua Video:

  1. Zilizoteuliwa: Video hizi ni kwa ajili ya mambo fulani hususa, kama vile zile zilizoteuliwa kwa ajili ya mikutano yetu ya kila juma au ibada ya familia.

  2. Video za Karibuni: Video zilizoongezwa hivi karibuni.