JW BROADCASTING
Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi—JW Broadcasting (Roku)
Huenda hautafuti maneno sahihi katika sehemu ya Tafuta. Angalia maelekezo ya Kusakinisha JW Broadcasting. Sababu nyingine ni huenda kifaa chako hakitegemezwi kwa sasa. JW Broadcasting inafanya kazi kwenye Roku LT, Roku 1, Roku 2, Roku 3, na Roku Streaming Stick.
Ili kupata orodha ya lugha zinazopatikana kwenye Roku. Fungua sehemu ya Mipangilio katika ukurasa wa mwanzo na utumie sehemu ya Chagua Lugha.
Unaweza kupakua na kutumia programu ya JW Broadcasting bila malipo.
Kadi ya benki inahitajika kufungua akaunti ya Roku kwa sababu vipindi vingine kwenye King’amuzi cha Roku vinatozwa. Utavilipia ukiamua kuvinunua. Kwa habari zaidi, tembelea Sehemu ya utegemezo kwenye Tovuti ya Roku.
Kwa sasa sehemu ya Onyesha Maandishi ya Video haipatikani katika video fulani zilizowekwa hivi karibuni kwenye JW Broadcasting katika king’amuzi cha Roku, na haitapatikana kwa miezi kadhaa. Watumiaji wa Roku wanaotumia maandishi ya video, wanaweza kuyaona kwenye kompyuta au kifaa cha mkononi kupitia tovuti ya tv.pr418.com. Ili kuona maandishi hayo, chagua sanduku Onyesha maandishi ikiwa yapo kwenye sehemu ya Vipimo.
Rafiki anayejua jinsi ya kutumia Roku au JW Broadcasting anaweza kukusaidia. Ikiwa swali lako linahusiana na kifaa chako cha Roku au akaunti, tembelea utegemezo wa Roku mtandaoni. Ikiwa tatizo lako linahusu programu ya JW Broadcasting, tafadhali jaza na utume fomu yetu ya msaada mtandaoni.