JW LIBRARY
Tumia Sehemu ya Zitakazochezwa
Katika tabo ya Funzo la Kibinafsi, unaweza kuunda orodha ya video, rekodi za sauti, na picha. Kwa mfano, unaweza:
Kuwa na kipengele chenye nyimbo za kitheokrasi unazopenda ambazo zinaweza kuchezwa kwa mfuatano
Kukusanya video na picha utakazotumia katika huduma
Kutayarisha orodha ya picha kwa ajili ya hotuba yako na kushiriki orodha hiyo pamoja na ndugu wanaosaidia katika mfumo wa sauti na video
Unda Kipengele cha Zitakazochezwa
Badili Habari Kwenye Kipengele
Unda Kipengele cha Zitakazochezwa
Unda Zitakazochezwa
Nenda kwenye Funzo la Kibinafsi > Zitakazochezwa
Bofya Ongeza Kwenye Zitakazochezwa yenye alama ya jumlisha
Chagua aidha Unda Zitakazochezwa au Pakia Zitakazochezwa
Unda Zitakazochezwa: Andika jina kwa ajili ya kipengele unachounda kisha bofya Unda
Pakia Zitakazochezwa: Chagua faili katika kifaa chako ambayo utaongezea kwenye kipengele
Ongeza Kwenye Kipengele cha Zitakazochezwa
Video, muziki, na rekodi nyingine za sauti kwenye programu
Bofya alama ya Mengineyo
Bofya Ongeza Kwenye Zitakazochezwa
Chagua kipengele mojawapo ikiwa kipo au bofya Unda Zitakazochezwa ili kuunda kipengele
Picha zinazopatikana ndani ya programu ya JW Library
Chagua picha
Bofya Ongeza Kwenye Zitakazochezwa kwenye alama ya jumlisha
Chagua kipengele mojawapo ikiwa kipo au bofya Unda Zitakazochezwa ili kuunda kipengele
Vyanzo Vingine
Unaweza kuongeza video, rekodi za sauti, au picha kwenye zitakazochezwa.
Nenda kwenye ukurasa wa Zitakazochezwa
Fungua kipengele ulichounda awali
Bofya Pakia Faili
Chagua faili unayotaka kuongeza kwenye kipengele hicho
Badili Habari Kwenye Kipengele
Badili Jina
Badili jina la kipengele:
Ikiwa umefungua sehemu ya Zitakazochezwa, bofya alama ya Mengineyo kwenye kipengele, kisha chagua Badili Jina na uandike jina unalotaka
Ikiwa umefungua kipengele fulani, bofya alama ya Badili Jina kisha uandike jina unalotaka
Badili jina la video, rekodi ya kusikiliza, au picha iliyo ndani ya kipengele:
Bofya alama ya Mengineyo kwenye video, rekodi ya kusikiliza, au picha hiyo
Chagua Badili Jina kisha andika jina jipya
Badili Mfuatano wa Video, Rekodi za Kusikiliza, na Picha Ndani ya Kipengele
Shikilia unachotaka kuhamisha kisha ukiachilie unapofika unapotaka kukihamishia
Kuwezesha Video
Video, rekodi ya kusikiliza, au picha inapofunguliwa katika kipengele huwa inaanza kucheza moja kwa moja. Unaweza kubadili hilo kwenye Vipimo. Kuna machaguzi mawili, Cheza na Sitisha.
Kubadili Mipangilio
Unaweza kuamua kubadili mpangilio wa video na rekodi za sauti zinapomaliza kucheza:
Bofya Endelea
Chagua kati ya Endelea, Simamisha, Gandisha, na Rudia
Endelea ndio mpangilio uliopo. Unaweza kubadilisha mpangilio huo wa msingi kwenye Mipangilio.
Umalizio |
Simamisha, Gandisha, na Rudia |
---|---|
Endelea |
Itacheza kinachofuata katika kipengele hicho |
Simamisha |
Kinachocheza kitakapofika mwisho itarudi orodha ya vitu katika kipengele |
Gandisha |
Kinachocheza kitakapofika mwisho kinachofuata hakitacheza |
Rudia |
Kinachocheza kinaendelea kujirudia upya |
Punguza Urefu wa Rekodi
Unaweza kupunguza urefu wa rekodi kwa kutumia Kata ili kuchagua kisehemu unachotaka cha video au rekodi ya sauti.
Bofya alama ya Mengineyo iliyo kulia juu kwenye rekodi hiyo kisha chagua Kata
Au, ikiwa unacheza rekodi, nenda kwenye kitufe cha Mipangilio kisha chagua Kata
Punguza kisanduku kinachoonyesha muda kwa kukivuta kushoto hadi sehemu rekodi itakapoanzia au kulia hadi sehemu itakapoishia
Ili kupatia muda kamili wa kuanzia au kuishia, tumia kistari cheupe kilicho ndani ya kisanduku hicho
Cheza kisehemu hicho ulichopunguza kwa kubofya Cheza
Kushiriki Kipengele cha Zitakazochezwa
Unaweza kushiriki kipengele ulichounda.
Ikiwa umefungua ukurasa wa Zitakazochezwa, bofya alama ya Mengineyo kwenye kipengele hicho, kisha bofya Shiriki na uchague programu utakayotumia ili kushiriki kipengele hicho
Ikiwa umefungua kipengele, bofya Shiriki na uchague programu utakayotumia ili kutuma kipengele hicho
Njia za Mkato za Kibodi
Njia za mkato za kibodi ni njia rahisi ya kubadili video, rekodi za sauti, au picha zinazochezwa katika kipengele.
Windows |
macOS |
|
---|---|---|
Kurudia iliyotangulia |
Page Up |
Mshale wa Juu |
Cheza inayofuata |
Page Down |
Mshale wa Chini |