Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW LIBRARY

Pakua na Utumie Machapisho​—iOS

Pakua na Utumie Machapisho​—iOS

Kwenye JW Library, unaweza kusoma vitabu, broshua, na trakti, na kutazama video nyingi hata bila kuunganishwa kwenye Intaneti.

Fuata maelekezo yafuatayo ili kupakua na kutumia machapisho:

 Pakua Chapisho

Unaweza kupakua machapisho mengi kadiri unavyotaka ili usome na kujifunza unapozima Intaneti.

  • Bofya tabo ya Machapisho ili kuona orodha ya machapisho.

  • Ukibofya kitufe cha Lugha utaona orodha ya lugha ambazo machapisho yanapatikana. Chagua lugha unayotaka kutumia. Lugha unazotumia mara nyingi zitapangwa juu kwenye orodha hiyo. Unaweza pia kutafuta lugha kwenye orodha hiyo kwa kuandika jina la lugha hiyo.

Kuna njia kadhaa za kutafuta machapisho unapotumia JW Library.

Sehemu inayoitwa Aina inaonyesha machapisho katika lugha uliyochagua yakiwa yameorodheshwa kwa aina, kama vile vitabu, trakti, au video. Ukibofya aina fulani ya machapisho utapata uchaguzi wa ziada, kwa mfano ukibofya Mnara wa Mlinzi utapata mpangilio kwa kutegemea mwaka au sehemu ya video itakupa aina mbalimbali za video. Ukibofya sehemu iliyoandikwa Aina Zote itakurudisha kwenye orodha ya machapisho yote.

Sehemu ya Nini Kipya inaonyesha machapisho ambayo yametolewa hivi karibuni katika lugha uliyochagua.

Machapisho ambayo bado hayajapakuliwa yana alama ya wingu. Bofya chapisho ikiwa unataka kulipakua. Chapisho hilo linapomaliza kupakuliwa, alama ya wingu hupotea. Bofya chapisho hilo ili uweze kulisoma.

Sehemu inayoitwa Zilizopakuliwa inaonyesha machapisho yote ambayo umepakua katika lugha yoyote. Unaweza kuyapanga machapisho kwa njia nne. Njia ya kwanza ni Kichwa, pili, Unazotumia kwa Ukawaida, tatu, Ambazo Hutumii kwa Ukawaida, au nne, Kubwa Zaidi.

 Futa Chapisho

Unaweza kufuta chapisho ikiwa hulihitaji tena au ikiwa unahitaji nafasi zaidi kwenye kifaa chako.

Bofya tabo ya Machapisho, kisha ubofye aina ya chapisho (kwa mfano, Vitabu) ili kuona orodha ya machapisho. Bofya kitufe cha Chagua, kisha bofya chapisho unalotaka kufuta. Unaweza pia kubonyeza chapisho kwa muda mrefu ili kulichagua. Bofya kitufe cha Ondoa, kisha thibitisha kwamba unataka kufuta chapisho hilo.

Ikiwa unahitaji kupata nafasi zaidi kwenye kifaa chako, unaweza kufuta machapisho usiyotumia kwa ukawaida au machapisho makubwa sana. Fungua orodha ya kurambaza, na ubofye sehemu iliyoandikwa Machapisho. Bofya sehemu ya Zilizopakuliwa, kisha panga orodha hiyo kulingana na Ambazo Hutumii kwa Ukawaida au Kubwa Zaidi. Futa machapisho ambayo huhitaji.

 Sasisha Chapisho

Mara kwa mara, machapisho ambayo tayari umepakua hurekebishwa au matoleo mapya kuingizwa.

Chapisho ambalo limerekebishwa huwa na alama ya vishale.Unapobofya chapisho hilo, utaona ujumbe unaosema kwamba chapisho hilo limerekebishwa. Bofya Pakua ili kulisasisha, au ubofye Baadaye ili kuendelea kusoma chapisho ulilopakua tayari.

Ili uone ikiwa chapisho lolote ulilopakua limerekebishwa, bofya tabo ya Machapisho. Ikiwa kuna machapisho yaliyorekebishwa, sehemu ya Sasisha itaonekana. Ukiibofya utaona orodha ya machapisho yote yanayohitaji kusasishwa. Bofya chapisho moja ili kulisasisha, au ubofye kitufe cha Sasisha Zote ili upakue machapisho yote yaliyorekebishwa.

Sehemu hizo mbalimbali zilipatikana Februari 2015 kwenye JW Library toleo la 1.4, ambalo linafanya kazi vizuri kwenye vifaa vinavyotumia mfumo wa iOS 6.0 au wa karibuni zaidi. Ikiwa hauoni mambo haya, tafadhali fuata mwelekezo kwenye makala “Anza Kutumia JW Library​—iOS,” kwenye Pata Habari za Karibuni Zaidi.