Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW LIBRARY

Tumia Historia​—Windows

Tumia Historia​—Windows

JW Library inahifadhi historia ya makala na sura za Biblia unazosoma. Hilo linaweza kuwa na faida, kwa mfano, unapotaka kurudi kwenye andiko ulilokuwa umesoma mapema.

Fuata maelekezo yafuatayo ili kutumia Historia:

 Fungua Orodha ya Historia

Fungua Amri za Programu, kisha bofya kitufe cha Historia ili uone orodha ya maandiko na makala ambazo umesoma hivi karibuni. Bofya andiko au makala katika orodha ya historia ili uisome tena.

 Futa Historia

Fungua Amri za Programu kwa kubonyeza upande wa kulia wa kipanya au nenda upande wa chini wa skrini. Bofya kitufe cha Historia ili ufungue orodha ya historia. Bofya kitufe cha Futa ili ufute kila kitu kwenye orodha hiyo.

Sehemu hizo mbalimbali zilipatikana Machi 2014 kwenye JW Library toleo la 1.1, ambalo linafanya kazi vizuri kwenye vifaa vinavyotumia mfumo wa Windows 8.0 au wa karibuni zaidi. Ikiwa huoni mambo haya, tafadhali fuata mwelekezo kwenye makala “Anza Kutumia JW Library​—Windows,” kwenye Pata Habari za Karibuni Zaidi.