JW LIBRARY
Sakinisha JW Library Ikiwa Huwezi Kuipakua Kwenye (App Store) Ukitumia Kifaa cha Windows
Ikiwa huwezi kusakinisha JW Library kwenye kifaa chako cha Windows kutoka kwenyeMicrosoft Store, unaweza kuisakinisha kwa kutumia faili za kusakinisha za JW Library Windows.
Huenda ukahitaji kubadili mipangilio ya kifaa chako ili iruhusu kifaa chako kusakinisha programu kutoka kwa vyanzo vingine. Nenda kwenye Mipangilio (Setttings) kisha fungua sehemu yenye mipangilio kutoka kwa watengenezaji(developers). Kisha, bonyeza chaguo linaloruhusu kusakinisha programu kutoka kwenye chanzo chochote au vyanzo vingine. Zingatia: Ikitegemea toleo la Windows unalotumia huenda chaguo hilo likawa na maneno kama vile, “Developer Mode” au “Sideload apps.”
Pakua na usakinishe faili za kusakinisha za JW Library Windows:
Bofya kitufe cha Pakua katika ukurasa huu ili kuhifadhi faili za kusakinisha kwenye diski ya kompyuta.
Bofya kitufe cha kulia kwenye kipanya chako ili ufungue faili ya zip.
Fungua folda, tumia kitufe cha kulia cha kipanya chako kubofya kwenye faili ya Install.ps1, kisha bofya Run with PowerShell.
Thibitisha kwamba cheti cha kusaini kimesakinishwa ikiwa kinahitajika.
Baada ya kumaliza kusakinisha ujumbe wa uthibitisho utatokea.
Mara kwa mara angalia ikiwa kuna toleo jipya la programu ya JW Library.
Fungua ukurasa wa Mipangilio kwenye JW Library ili kuona kifaa chako kina toleo gani la programu hiyo.
Ikiwa namba ya toleo inayoonyeshwa kwenye Mipangilio ni tofauti na namba iliyo hapa chini, pakua na kusakinisha programu ya JW Library kwa kufuata hatua zilizotajwa hapo juu.
Version: 14.3.45 (429479)