Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

TOVUTI YA JW.ORG

Jinsi ya Kunufaika Zaidi na Video Katika Kifaa Chako

Jinsi ya Kunufaika Zaidi na Video Katika Kifaa Chako

Nenda kwenye MAKTABA > VIDEO ili kuona video zote zilizopo. Kuna vipengele kadhaa na kila kipengele kimegawanyika katika vipengele vingine.

 Cheza, Tua, Peleka Mbele, na Rudisha Nyuma

 Tumia Ishara Kwenye Simu-Janja

 Badilisha Mipangilio ya Video

 Cheza, Tua, Peleka Mbele, na Rudisha Nyuma

Video inapoendelea kucheza, unaweza kutokeza alama za kuichezesha kwa kugusa skrini au kwa kusogeza kipanya juu ya video.

Kitufe

Kazi Inayofanya

Rudi Nyuma 5

Video itarudi nyuma kwa sekunde 5

Peleka Mbele 15

Video itaenda mbele kwa sekunde 15

Iliyotangulia

Ikiwa video ilianza kucheza itarudi mwanzo, au itacheza video iliyotangulia

Inayofuata

Itacheza video inayofuata

Zima Sauti/Rudisha Sauti

Hutoa sauti au kuirudisha

Kuza Video/Punguza Video

Hukuza ukubwa wa video ili kujaza skrini nzima au kuipunguza iwe ndogo ikiwa ilikuwa imejaza skrini

 Tumia Ishara Kwenye Simu-Janja

Kwenye simu-janja (isipokuwa simu za Apple), tumia ishara zifuatazo ili kucheza, kutua, kupeleka mbele, au kurudisha nyuma:

Kusudi

Ishara

Cheza au Tua

Gusa kwa vidole 2

Rudi nyuma sekunde 5

Gusa mara mbili upande wa kushoto wa video

Peleka mbele sekunde 15

Gusa mara mbili upande wa kulia wa video

 Badilisha Mipangilio ya Video

Bofya Mipangilio:

  • Bofya kitufe cha Maandishi ya Video (Subtitles) ili yatokee au ili kuyatoa ikiwa yanapatikana.

  • Chagua Kasi (Speed) ili kubadili kasi ya video

  • Chagua Ubora (Quality) ili kuchagua ubora wa mwonekano wa video. Namba ndogo hucheza video hata Intaneti isipokuwa na kasi. Namba kubwa hufaa skrini kubwa