Sera ya Faragha
MUHIMU: KWA KUTUMIA TOVUTI YETU NA PROGRAMU YOYOTE ILIYOTAYARISHWA NA WATCHTOWER BIBLE AND TRACT SOCIETY OF NEW YORK, INC. NA/AU KUTUPATIA HABARI ZAKO ZA KIBINAFSI, UNAKUBALI KWAMBA HABARI ZOTE ZA KIBINAFSI ULIZOTUMA ZINAWEZA KUTUMIWA KUTIMIZA MAKUSUDI YALIYOELEZWA KWENYE SERA YA FARAGHA IFUATAYO KULINGANA NA SHERIA NA TARATIBU ZA HABARI ZA KIBINAFSI.
Sera ya Ujumla ya Faragha
Ona Pia
KUHESHIMU FARAGHA YAKO
Tuna wajibu wa kulinda na kuheshimu faragha yako. Sera hii inaonyesha msingi wa kutumia taarifa zozote za kibinafsi tunazochukua kutoka kwako au zile unazotupatia katika tovuti yetu na katika programu yoyote iliyotayarishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc. (“Watchtower”). Tunahifadhi baadhi ya taarifa za msingi unapotembelea tovuti yetu na tunatambua umuhimu wa kulinda usalama wa taarifa hizo na kukujulisha tutazifanyia nini. Unaweza kuamua kutupatia taarifa zile unazoona kuwa ni taarifa za kibinafsi. Neno “taarifa za kibinafsi” linalotumiwa katika sera hii linarejelea taarifa kama vile jina lako, anwani ya barua pepe, anwani ya posta, namba ya simu, au taarifa nyingine yoyote ambayo inaweza kutumiwa kukutambulisha. Neno “tovuti” linatia ndani tovuti hii na nyingine zinazohusiana na hii, kama vile apps.pr418.com, ba.pr418.com, stream.pr418.com, na wol.pr418.com.
WANAOTUMIA TAARIFA ZAKO
Tovuti hii pamoja na programu yoyote iliyotayarishwa na Watchtower ni mali ya Watchtower, ambalo ni shirika lisilo la kibiashara lililoko jijini New York linalotegemeza utendaji wa Mashahidi wa Yehova na elimu yao ya Biblia. Ikiwa umeamua kwa hiari yako kufungua akaunti, kutoa mchango, kuomba kutembelewa, au kufanya jambo lolote ambalo linahitaji ueleze taarifa zako za kibinafsi, unaonyesha unakubaliana na Sera hii, pamoja na kukubali taarifa zako zihifadhiwe kwenye vifaa vilivyoko Marekani na taarifa zako za kibinafsi zikusanywe, zishughulikiwe, zihamishwe na kutunzwa na Watchtower na mashirika mengine yanayohusiana nayo ambayo yanategemeza Mashahidi wa Yehova katika nchi mbalimbali kama zinavyohitajiwa ili kushughulikia ombi lako. Shirika hilo la kidini linafanya kazi ulimwenguni pote kupitia mashirika mbalimbali ya kisheria. Kwa kusudi la kulinda taarifa, sehemu nyingine zinazohusika zinatia ndani makutaniko, ofisi za tawi, na mashirika mengine yanayohusiana na Mashahidi wa Yehova.
Wanaotumia taarifa zako za kibinafsi wanatofautiana ikitegemea kile unachohitaji katika tovuti. Kwa mfano, ikiwa unachangia shirika la kisheria katika nchi fulani, jina lako na taarifa zako za mawasiliano zitapelekwa kwenye shirika hilo la kisheria kama ilivyoonyeshwa wakati ukituma mchango wako. Mfano mwingine, ikiwa unaomba kutembelewa, jina lako na taarifa zako za mawasiliano zitapelekwa kwenye ofisi ya tawi ya kwenu na kutaniko la Mashahidi wa Yehova ili kutimiza ombi lako.
Ili kukusaidia, ikiwa katika nchi unayoishi kuna sheria za kulinda taarifa za kibinafsi zinazotumika, unaweza kupata taarifa za mawasiliano kwa ajili ya nchi unayoishi katika ukurasa wa Watu Wanaolinda Taarifa.
USALAMA NA USIRI WA TAARIFA
Tunahakikisha kwamba taarifa zako za kibinafsi zipo salama. Mifumo yetu ya kuhifadhi na kulinda taarifa zako za kibinafsi inaboreshwa mara kwa mara ili taarifa zako zisitumiwe bila ruhusa, zisitumiwe vibaya, zisibadilishwe bila ruhusa, zisifutwe kinyume cha sheria, au zisipotee. Mtu yeyote wa tatu atakayeshughulika na taarifa zako za kibinafsi na wote wanaoshughulikia taarifa zako za kibinafsi na wana wajibu wa kuheshimu usiri wa taarifa zako. Tunatunza taarifa zako za kibinafsi kwa muda zinapohitajika tu na kwa kusudi la kukusanywa au kwa kuzingatia ripoti yoyote ya kisheria inayohusika au matakwa ya kutunza taarifa yaliyoko kwenye hati.
Tunalinda taarifa zako za kibinafsi zinapokuja kwa kutumia mifumo ya kiteknolojia, kama, teknolojia ya Transport Layer Security (TLS). Tunatumia mifumo ya kompyuta inayotumiwa na watu wachache inayolindwa kielektroni kwa kutumia mikakati hususa iliyowekwa ili kulinda usiri na usalama wa taarifa za kibinafsi zinazotufikia. Tuna viwango imara vya usalama vinavyozuia matumizi yoyote ya taarifa bila kibali.
WATOTO
Ikiwa wewe ni mtoto kulingana na sheria ya nchi unayoishi na unatumia tovuti yetu, unaweza kutuma taarifa zako za kibinafsi katika tovuti hii ikiwa tu utamhusisha mzazi au mlezi wako. Ikiwa wewe ni mzazi au mlezi nawe umekubali mtoto atoe taarifa za kibinafsi katika tovuti hii, unaonyesha umekubali Sera hii kwa ajili ya matumizi ya mtoto huyo.
TAARIFA KWA MTU WA TATU
Nyakati nyingine, tovuti hii na programu yoyote iliyotayarishwa na Watchtower zinaweza kutumia viunganishi vinavyokuelekeza kwa mtu wa tatu. Hilo linaweza kutia ndani viunganishi kwa tovuti nyingine ya mtu wa tatu (third-party) inayotoa huduma fulani kwa niaba yetu (kwa mfano, inapohusu kujaza fomu mtandaoni). Utatambua kwamba umeingia kwenye tovuti nyingine kwa sababu mwonekano wa tovuti hiyo utakuwa tofauti na anwani ya tovuti itabadilika. Kwa kuongezea, wanaweza kukutumia barua pepe au ujumbe kwenye simu yako kutokana na ombi ulilojaza katika tovuti hii na wanaweza kukujulisha kuhusu mambo ambayo ulikuwa unafanya kulingana na taarifa ulizojaza kupitia tovuti hii. Wakati tunapomchagua mtu wa tatu wa kutoa huduma, na mara kwa mara baada ya hapo, tunachunguza sera zao za faragha na za kulinda taarifa za kibinafsi ili kuhakikisha kwamba zina viwango vinavyofanana na vile tunavyotumia katika sera zetu. Hata hivyo, tovuti hizo nyingine hutoa program na huduma ambazo muundo wake, masharti ya utumiaji, sera za faragha, na mambo mengine yanayohusiana na utumiaji ambayo hatuwezi kudhibiti. Kwa sababu hiyo, utumiaji wako wa programu na huduma hizo ndani ya tovuti yetu utategemea masharti ya huduma yaliyopo wakati huo na matumizi ya tovuti hiyo kwa ujumla. Tovuti hizo zinaposasisha taarifa zao hazitujulishi, hivyo basi pitia masharti ya utumiaji kabla ya kutumia huduma zao. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu sera za tovuti hizo za kutoa huduma, tafadhali soma sera inayopatikana kwenye tovuti yao.
Utumiaji wako wa Huduma ya Ramani ya Google (Google Maps) katika tovuti yetu unategemea sera ya faragha ya Google; Google Privacy Policy. Google ni mtu wa tatu ambaye programu, muundo na masharti yake; Terms of Service kwa ujumla yako nje ya uwezo wetu. Kwa hiyo, utumiaji wako wa Huduma ya Ramani ya Google (Google Maps) uko chini ya Masharti Zaidi ya Huduma ya Ramani ya Google Google Maps/Google Earth Additional Terms of Service Hawatujulishi kuhusu usasishaji wa huduma zao, hivyo basi tafadhali pitia masharti ya utumiaji kabla ya kutumia huduma hiyo. Usitumie Huduma ya Ramani ya Google ikiwa hukubaliani na masharti ya utumiaji.
KUJULISHWA KUHUSU MABADILIKO YA SERA
Tunaendelea kuboresha na kuongeza utendaji mpya na mambo mengine katika tovuti hii na programu nyingine zilizotayarishwa na Watchtower, na pia tunaboresha na kuongeza huduma nyingine. Kwa sababu ya mabadiliko yanayoendelea, na mabadiliko ya sheria na teknolojia, tunaweza kubadili jinsi tunavyotumia habari mara kwa mara. Tukihitaji kubadili Sera yetu, tutaonyesha mabadiliko hayo kwenye ukurasa huu ili sikuzote ujue habari tunazokusanya na jinsi tunavyozitumia.
HATIJAVA (ACTIVE SCRIPTING AU JAVASCRIPT)
Hati hutumiwa na tovuti kuboresha utendaji wa tovuti na programu yoyote iliyotayarishwa na Watchtower. Kutumia ufundi wa hati hutuwezesha kurejesha haraka zaidi habari ulizoomba. Hati haitumiwi kamwe na tovuti au programu yoyote iliyotayarishwa na Watchtower kusakinisha programu kwenye kompyuta ya mtumiaji wala kukusanya habari kutoka kwa mtumiaji pasipo idhini.
Katika tovuti yetu, ni muhimu HatiJava iwezeshwe katika kivinjari chako ili sehemu fulani za tovuti zifanye kazi ifaavyo. Vivinjari vingi humruhusu mtumiaji kuwezesha au kulemaza hati hizo katika tovuti hususa. Soma habari za msaada kuhusu kivinjari chako ili upate kujua jinsi ya kuwezesha hati katika tovuti teule.