Hamia kwenye habari

Matumizi ya Habari za Kibinafsi​—Slovakia

Matumizi ya Habari za Kibinafsi​—Slovakia

Ukurasa huu wa taarifa za faragha unafafanua jinsi gani na kwa nini Mashahidi wa Yehova hukusanya na kutumia taarifa za kibinafsi za wahubiri, na unaeleza haki za wahubiri kuelekea taarifa zao za kibinafsi. Inapotajwa “wewe” inarejelea mhubiri a ambaye hajabatizwa au aliyebatizwa ambaye yuko katika kutaniko la Mashahidi wa Yehova na taarifa zake za kibinafsi zinashughulikiwa na Mashahidi wa Yehova inapohusu kudumisha na kuendeleza dini na utendaji wa kidini wa Mashahidi wa Yehova. Mashahidi wa Yehova wanapatikana ulimwenguni pote. Katika ukurasa huu, maneno “Shirika la Kidini,” au “sisi,” yanarejelea shirika la kidini la ulimwenguni pote la Mashahidi wa Yehova au yanarejelea mashirika yanayotumiwa na Mashahidi wa Yehova kama vile kutaniko la eneo fulani, ofisi ya tawi, na kadhalika. Mashirika hayo yanahusika moja kwa moja katika kushughulikia taarifa zako za kibinafsi, ikitegemea msingi wa kutoa taarifa zako. Shirika la Kidini la Mashahidi wa Yehova katika Jamhuri ya Slovakia ndilo linaloshughulikia taarifa za wahubiri walio katika makutaniko yaliyo nchini Slovakia. Kama inavyoelezwa katika kitabu Tengenezo Linalofanya Mapenzi ya Yehova, tunakusanya taarifa zako za kibinafsi kutoka kwako, kutoka kwa taarifa za umma, au kutoka kwa wengine mara unapokuwa mhubiri ili uweze kushiriki utendaji wa kidini unaohusiana na ibada yako na pia ili upate msaada wa kiroho.​—1 Petro 5:2.

Ikiwa una maswali yoyote kuhusu matumizi ya taarifa zako za kibinafsi au ikiwa ungependa kuwasiliana na ofisa anayeshughulikia masuala ya kulinda taarifa katika eneo lenu, tafadhali tuma barua pepe kwenye anwani ifuatayo:DataProtectionOfficer.SK@jw.org.

Utapata habari zaidi kuhusu matumizi ya taarifa zako za kibinafsi hapa chini.

Taarifa zako za kibinafsi tunazokusanya

Habari za kibinafsi unazotupatia zinatusaidia kudumisha na kusimamia utendaji wa kidini wa Mashahidi wa Yehova. Kwa sababu hiyo, utaona kwamba habari za kibinafsi tunazokusanya ni za kawaida. Habari hizo zinatia ndani habari zifuatazo:

  • Taarifa za msingi, kama vile jina lako tarehe ya kuzaliwa, na jinsia yako

  • Taarifa za mawasiliano,  kama vile anwani yako ya posta, anwani ya barua pepe, namba za simu, na watu tunaoweza kuwapigia ukipata dharura

  • Taarifa za mambo ya kiroho, kama vile tarehe yako ya kubatizwa, ikiwa wewe ni “mtiwa-mafuta” au kati ya “kondoo wengine,” jukumu au mgawo wowote ulio nao katika kutaniko lenu au katika Tengenezo letu la Kidini, utendaji wako katika huduma ya shambani, hali yako ya kiroho na tarehe zozote zinazohusiana na mabadiliko yoyote ya kiroho pamoja na habari nyingine zozote kuhusu hali yako ya kiroho.

Taarifa za kibinafsi tunazokusanya kukuhusu zinaweza kutia ndani makundi maalum ya taarifa za kibinafsi (au kundi maalum la taarifa za kibinafsi). Makundi hayo yanatia ndani kabila lako na imani yako ya kidini pamoja na mambo mengine.

Kusudi na msingi wa kisheria wa kutumia taarifa zako za kibinafsi

Sera yetu ni kukusanya taarifa za kibinafsi tunazohitaji tu ili kutimiza kusudi letu na kufanya hivyo kwa kuzingatia sheria.

Unapokuwa mhubiri, tunakusanya na kutumia taarifa zako za kibinafsi kupatana na sheria tukiwa na kusudi la kudumisha na kuendeleza dini ya Mashahidi wa Yehova na hilo linakuwezesha kushiriki katika utendaji wa kidini unaohusiana na ibada yako na kupokea msaada wa kiroho. Ikiwa tutatambua kwamba tunahitaji kuweka taarifa zako za kibinafsi kwenye kikundi maalum kama vile imani yako ya kidini, tutashughulikia taarifa zako kwa kuzingatia tahadhari bila kufunua taarifa hizo nje ya Tengenezo la Kidini isipokuwa kwa ruhusa yako. Tunachanganua kwa makini athari zozote zinazoweza kukupata na tunazingatia haki zako kabla ya kushughulikia taarifa zako za kibinafsi tunapotimiza kusudi letu..

Pia, tunaweza kutumia taarifa zako za kibinafsi ili kutimiza wajibu fulani wa kisheria. Katika hali ya dharura huenda tukatumia taarifa zako za kibinafsi kwa ajili ya masilahi yako ya kibinafsi au ya mtu mwingine. Kwa ujumla, hatushughulikii taarifa kwa kutegemea ruhusa ya mtu binafsi kwa sababu tunategemea msingi mwingine wa kisheria. Hata hivyo, tunaweza kutegemea ruhusa yako ikiwa umetoa idhini ya moja kwa moja ya kutumia taarifa zako. Tafadhali zingatia kwamba taarifa za kibinafsi za watoto walio chini ya umri wa miaka 18 hazishughulikiwi bila ruhusa ya mzazi au mlezi anayetambulika kisheria..

Jedwali lifuatalo linafafanua jinsi tunavyotumia taarifa zako za kibinafsi na msingi wa kisheria unaotuongoza. Tafadhali wasiliana na ofisa anayeshughulikia masuala ya kulinda taarifa katika eneo lenu kwa kutumia habari za mawasiliano zilizo hapo juu ikiwa unahitaji kujua mengi zaidi.

Kusudi na/au utendaji

Aina ya taarifa

wa kisheria wa kuishughulikia

Itahifadhiwa kwa muda gani

  • Kuhifadhi Rekodi ya Kutaniko ya Mhubiri (rekodi za mhubiri zinazohusu mambo ya kiroho)

  • Taarifa za msingi

  • Taarifa za mambo ya kiroho

  • Makundi maalum ya taarifa za kibinafsi: imani ya kidini

  • Masilahi ya kisheria: kudumisha na kuendeleza dini au utendaji wa kidini wa Mashahidi wa Yehova

  • Wahubiri wanaotenda:Rekodi za mwaka huu wa utumishi na mwaka uliotangulia

  • Wahubiri wasiotenda: Rekodi za mwaka wa utumishi wa mwisho ambao walikuwa wakitenda

  • Rekodi za wale ambao wameacha kuwa Mashahidi wa Yehova hazihifadhiwi

  • Zingatia: mwaka wa utumishi huanza Septemba na kukamilika Agosti

  • Kushiriki katika mikutano, kazi za kujitolea, au miradi ya Mashahidi wa Yehova

  • Taarifa za msingi

  • Katika baadhi ya kazi za kujitolea au miradi: Taarifa za mawasiliano na baadhi ya taarifa za kiroho

  • Makundi maalum ya taarifa za kibinafsi: imani ya kidini

  • Masilahi ya Kisheria: kudumisha na kuendeleza dini au utendaji wa kidini wa Mashahidi wa Yehova

  • Hakuna rekodi kuhusu kushiriki mikutano

  • Huhifadhiwa kwa muda mrefu kadiri iwezekanavyo ili uweze kushiriki katika kazi za kujitolea au miradi

  • Kutimiza mgawo au jukumu katika kutaniko; hili linaweza kuhusisha habari zinazotia ndani jina lako, mgawo wako, au jukumu lako katika kutaniko, au kwa nadra katika Tengenezo la Kidini, habari zilizo kwenye ubao wa habari, au zinazopatikana kwa njia ya kielektroni kwa kuzingatia sheria zinazolinda taarifa zako

  • Taarifa za msingi

  • Baadhi ya taarifa za kiroho: jukumu au mgawo katika kutaniko lako au miongoni mwa Mashahidi wa Yehova

  • Makundi maalum ya taarifa za kibinafsi: imani ya kidini

  • Masilahi ya Kisheria: kudumisha na kuendeleza dini au utendaji wa kidini wa Mashahidi wa Yehova

  • Ratiba za mikutano ya kutaniko zinahifadhiwa hadi ratiba nyingine itakapoanza kutumiwa

  • Kutaniko linahifadhi habari za karibuni kuhusu migawo ya kikundi cha utumishi

  • Huhifadhiwa kwa muda mrefu kadiri iwezekanavyo kwa kutegemea kusudi na mgawo au jukumu

  • Uchungaji na msaada wa kiroho kutoka kwa wazee Mashahidi wa Yehova

  • Taarifa za msingi

  • Taarifa za mawasiliano

  • Taarifa za mambo ya kiroho

  • Makundi maalum ya taarifa za kibinafsi: imani ya kidini

  • Barua za kutambulishwa huhifadhiwa kupatana na sheria za eneo lenu

  • Huhifadhiwa kwa muda ambao zinaendelea kutimiza kusudi lake

  • Kushughulikia habari za mawasiliano wakati wa dharura

  • Taarifa za msingi

  • Taarifa za mawasiliano

  • Masilahi ya kibinafsi ya mhubiri. Mhubiri anawajulisha wale watakaopokea taarifa katika hali ya dharura.

  • Huhifadhiwa maadamu mhubiri yupo katika kutaniko hilo

  • Utendaji mwingine wowote ambao tunaona ni muhimu katika kudumisha na kuendeleza dini au utendaji wa kidini wa Mashahidi wa Yehova kupatana na sheria. (Ikiwa hili linatokea utajulishwa mapema kabla taarifa zako hazijashughulikiwa)

  • Taarifa za msingi

  • Taarifa za mawasiliano

  • Taarifa za mambo ya kiroho

  • Makundi maalum ya taarifa za kibinafsi: imani ya kidini

  • Masilahi ya Kisheria: kudumisha na kuendeleza dini au utendaji wa kidini wa Mashahidi wa Yehova; au

  • Wajibu wa kisheria; au

  • Ruhusa

  • Huhifadhiwa kwa muda mrefu kadiri iwezekanavyo au kupatana na matakwa ya sheria

Muda ambao rekodi zitahifadhiwa

Tunahifadhi rekodi za mtu kwa kipindi ambacho zinaweza kutumiwa tu kama ilivyoelezwa kwenye sehemu ya “Kusudi na msingi wa kisheria wa kutumia taarifa zako za kibinafsi” hapo juu.

Ili kuamua tuhifadhi taarifa za kibinafsi muda mrefu kadiri gani, tunazingatia matakwa ya kisheria yanayohusika, kiasi cha taarifa tulizo nazo, usiri wa taarifa hizo; madhara yanayoweza kutokea iwapo zitatumiwa bila ruhusa au kufunuliwa; kusudi letu la kushughulikia taarifa zako za kibinafsi na ikiwa tunaweza kutimiza kusudi letu kwa kutumia njia nyinginezo.

Muda wa kuhifadhi rekodi hizo unatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine kwa sababu unapatana na sheria za eneo hilo na muda uliowekwa na nchi wa kuhifadhi rekodi. Taarifa za kibinafsi zinaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu zaidi ikiwa sheria inaamuru hivyo na kwa kusudi la kufuatilia au kutetea haki zetu za kisheria.

Katika visa fulani, tunaweza kutumia taarifa zako za kibinafsi bila kutumia jina lako (ili watu wasijue kwamba ni wewe) katika utafiti au tunapokusanya takwimu. Katika hali kama hizo, tunaweza kutumia taarifa zako kwa muda mrefu zaidi bila kukujulisha.

Ikiwa ungependa kujua mengi zaidi kuhusu muda ambao rekodi zako za taarifa za kibinafsi zinahifadhiwa, tafadhali wasiliana na ofisa anayeshughulika na kulinda taarifa katika eneo lenu kwa kutumia taarifa za mawasiliano zilizo hapo juu.

Taarifa za kibinafsi zinavyozunguka

  • <uF0B7> Mashahidi wa Yehova wapo duniani pote. Kwa sababu hiyo, baadhi ya shughuli zetu kutia ndani huduma zinazohusu kushughulikia habari zinafanyiwa sehemu moja. Habari fulani zinatumiwa na mashirika mbalimbali ya Mashahidi wa Yehova kunapokuwa na uhitaji kupatana na makusudi yaliyozungumziwa katika makala hii na kama tu inavyoelezwa katika kitabu Tengenezo Linalofanya Mapenzi ya Yehova. Kwa mfano, ikiwa utaamua kuhamia kutaniko lingine, taarifa zako za kibinafsi (za msingi, mawasiliano, na taarifa za hali yako ya kiroho) zitahamishwa na kupelekwa kwenye kutaniko utakalohamia. Katika hali fulani, ofisi ya (za) tawi ya Mashahidi wa Yehova iliyo katika eneo lako itashughulikia taarifa zako ili uwe na uhuru wa kuendelea kushiriki kikamili katika utendaji wa kidini pamoja na kutaniko lako jipya, kwa njia hiyo nasi tutafaulu kuwa na habari za karibuni zaidi za wahubiri. Hili linaweza kutia ndani mtu anapohamia hata nchi ambazo hazimo katika Muungano wa Ulaya (EU)/ Eneo la Kiuchumi la Ulaya (EEA) na kwa nchi zisizo na sheria hususa zinazolinda habari za kibinafsi. Tunachukua tahadhari za kisheria na pia, hatua zinazofaa ili kulinda kwa uaminifu taarifa za kibinafsi zinazoingia kwenye Shirika letu la Kidini. Ikiwa upo katika Muungano wa Ulaya (EU)/ Eneo la Kiuchumi la Ulaya (EEA) tunaweza kuhamisha taarifa zako za kibinafsi tulizokusanya ikiwa mpokeaji yuko katika nchi ambayo inalinda taarifa zako za kibinafsi kwa kiwango kinachofaa; na/au

  • mpokeaji yuko chini ya makubaliano yanayokidhi matakwa ya EU ya kuhamisha taarifa za kibinafsi nje ya EU/EEA ili kushughulikiwa na mpokeaji. Makubaliano hayo ni kama mikataba inayohusiana na kulinda taarifa iliyopitishwa na Tume ya Ulaya; na/au

  • unapokubali mwenyewe.

Usalama wa Taarifa Zako

Tunalinda usiri wa taarifa zako tunazopata katika utendaji wetu. Ni watu wachache tu walioruhusiwa kuziona na tumeweka sera na utaratibu wa kulinda habari hizo ili zisipotee, zisitumiwe vibaya, au zisifunuliwe kwa mtu asiyehusika nazo.

  • Ili kuhakikisha kuna kiwango kinachofaa cha usalama tunaposhughulikia taarifa, tunazingatia mambo kama miundo mbinu ya usalama tuliyoweka katika shirika letu huku tukijitahidi kutumia teknolojia ya karibuni zaidi; gharama zinazohusika; aina ya habari, kiasi, mambo mengine yanayohusika, na kusudi la kushughulikia habari yenyewe; pia matumizi na matokeo ya habari hizo inapohusu haki za wanadamu. Tahadhari hizo zinatia ndani mambo yafuatayo: kudhibiti wanaoweza kupata habari hizo, kuhakikisha habari hizo hazivujishwi, na zinatumiwa kwa unyoofu;

  • usalama wa mawasiliano na utendaji;

  • kutumia mbinu mbalimbali ambazo zinalinda utambulisho wako ukiwa mtoa habari na pia kulinda habari zenyewe;

  • kuchanganua mara kwa mara ubora wa miundo mbinu inayotumiwa kuhakikisha taarifa ziko salama.

Kuwaelimisha wale walioruhusiwa kupata taarifa za kibinafsi kwa ukawaida kuhusu haki zao na majukumu yao.

Kufunua taarifa za kibinafsi

Tunaweza kuonyesha taarifa zako za kibinafsi katika hali zifuatazo:

  • ikiwa hilo linapatana na makusudi yaliyoelezwa katika sehemu ya “Kusudi na msingi wa kisheria wa kutumia taarifa zako za kibinafsi.” Hata katika Tengenezo letu;

  • ikiwa sheria inayotumika inadai hivyo;

  • ikiwa tunaamini kwamba kufunua taarifa hizo kunafaa ili kulinda haki, mali, au usalama wetu;

  • ikiwa taarifa hizo zinahitajika katika kesi inayoendelea mahakamani, mahakama imeziomba, au kuna sababu nyingine ya kisheria, au serikali au shirika lingine lililoidhinishwa kisheria limeomba taarifa hizo; au

  • ikiwa tumepata ruhusa yako.

Wanaoweza kupewa taarifa zako ni:

  • Mashirika ya Udhibiti

  • Mahakama, polisi, na vyombo vya kutekeleza sheria

  • Mashirika au watu wanaotoa huduma mbalimbali

Haki zako zinazotambulika kisheria kuhusiana na taarifa zako za kibinafsi

Huenda una haki fulani kulingana na sheria ya sehemu unayoishi kuhusu taarifa zako za kibinafsi tulizo nazo. Haki hizo ni kama:

  • Haki ya kujulishwa jinsi taarifa zako za kibinafsi zinavyotumiwa. Una haki ya kujulishwa jinsi tutakavyotumia taarifa zako za kibinafsi na ikiwa tutazitoa kwa njia yoyote ile.

  • Haki ya kuona taarifa zako za kibinafsi. Una haki ya kujulishwa ikiwa taarifa zako za kibinafsi zinashughulikiwa na pia una haki ya kuziona.

  • Haki ya kurekebisha taarifa za kibinafsi ambazo zina kosa lolote. Una haki ya kuomba kubadili taarifa zozote za kibinafsi au ambazo hazijakamilishwa. Kwa mfano, unapobadili taarifa zako za mawasiliano.

  • Haki ya kuomba habari za kibinafsi zifutwe katika hali fulani. Inajulikana pia kama “haki ya kusahaulika.” Hili halimaanishi kwamba ni lazima taarifa zote za kibinafsi zifutwe. Tutachanganua kila ombi au kuzingatia sheria zinazohusika.

  • Haki ya kukataa taarifa za kibinafsi zitumiwe. Ikiwa tungeshughulikia taarifa kwa kutegemea ruhusa ya mtu binafsi basi ungekuwa na haki ya kukataa muda wowote ule. Hata hivyo, kwa ujumla hatushughulikii taarifa kwa kutegemea ruhusa ya mtu binafsi kwa sababu tunategemea msingi mwingine wa kisheria.

  • Haki ya kudhibiti taarifa za kibinafsi zisishughulikiwe katika visa fulani. Unaweza kuomba zisishughulikiwe ikiwa unaona taarifa zako za kibinafsi si sahihi, ikiwa unataka zisishughulikiwe, ikiwa ni kinyume cha sheria kushughulikia taarifa za kibinafsi na hungependa zifutwe, hivyo unaomba zisishughulikiwe, au ikiwa hatuhitaji taarifa hizo tena lakini wewe unazihitaji kwa kusudi la kuzitumia mahakamani ili kufuatilia au kulinda haki fulani.

  • Haki ya kuhamisha taarifa. Haki ya kuhamisha taarifa inahusika tu ikiwa haki ya kuishughulikia inahitaji ruhusa yako au ikiwa ni lazima taarifa za kibinafsi zishughulikiwe ili mkataba uidhinishwe na ikiwa zinashughulikiwa kwa njia ya kielektroni.

  • Haki ya kukataa taarifa za kibinafsi zisishughulikiwe katika hali fulani. Una haki ya kukataa taarifa zako za kibinafsi zisishughulikiwe ikiwa tunashughulikia taarifa zako za kibinafsi kwa masilahi ya kisheria.

Unaweza kutumia haki hizi iwapo kuna jambo fulani kwa kuwasiliana na ofisa anayeshughulika na kulinda taarifa katika eneo lenu kwa kutumia taarifa za mawasiliano zilizo hapo huu.

Huenda tukahitaji kukuomba habari fulani hususa ili kuhakikisha ni wewe na kuwa na uhakika kwamba una haki ya kuona taarifa hizo (au ya kudai haki nyingine). Tunafanya hivyo kwa sababu ya usalama ili kuwa na uhakika kwamba hatufunui taarifa za mtu kwa mtu mwingine ambaye hana haki ya kuziomba. Huenda tukawasiliana na wewe moja kwa moja ili kupata habari zaidi zitakazotuwezesha kukupa jibu haraka zaidi.

Ikiwa unahisi kwamba Mashahidi wa Yehova wamekiuka sheria ya taarifa za kibinafsi au sheria nyingine yoyote, unaweza kuwasiliana na ofisa anayeshughulika na kulinda taarifa katika eneo lenu kwa kutumia taarifa za mawasiliano zilizo hapo huu. Ofisa huyo atafanya utafiti wa jambo hilo na kukueleza jinsi jambo hilo litakavyoshughulikiwa. Una haki pia ya kupeleka malalamiko yako kwa wenye mamlaka wanaohusika na kulinda taarifa katika nchi unayoishi, au katika sehemu ambapo tukio hilo lilitokea, au kwa mahakama husika.Mabadiliko katika ukurasa huu

Inawezekana utaratibu wa Mashahidi wa Yehova wa kushughulikia taarifa ukabadilika baada ya muda fulani kutokana na mabadiliko ya utendaji wa kidini, sheria, na teknolojia. Ikiwa kutakuwa na mabadiliko yoyote katika ukurasa huu wa Matumizi ya Taarifa za Kibinafsi, mabadiliko hayo yataonekana kwenye ukurasa huu ili wahubiri waweze kujua taarifa tunazokusanya na jinsi zinavyotumiwa. Tafadhali chunguza ukurasa huu mara kwa mara ili uone marekebisho yanayofanywa.

a Mhubiri ni mtu anayeshirikiana na kutaniko la Mashahidi wa Yehova na kuhubiri habari njema ya Ufalme wa Mungu.