Matumizi ya Taarifa za Kibinafsi—Makedonia Kaskazini
Taarifa za kibinafsi zinatia ndani jina, tarehe ya kuzaliwa, jinsia, tarehe ya kubatizwa, taarifa za mawasiliano, taarifa zinazohusiana na hali ya kiroho, utendaji katika kazi ya kuhubiri, daraka lolote ambalo mtu analo akiwa Shahidi wa Yehova, au taarifa zozote ambazo wahubiri wanatoa wanaposhiriki katika utendaji mwingine wowote wa kidini. Taarifa hizo zinatia ndani habari ambazo zinaonyesha imani ya kidini ya mhubiri na pia zinaweza kutia ndani taarifa nyingine za siri za kibinafsi. Matumizi ya taarifa za kibinafsi yanaweza kumaanisha kukusanya, kurekodi, kupanga, na kuhifadhi taarifa hizo, pamoja na njia nyingine yoyote inayofanana na hizo ya matumizi ya taarifa hizo.
Sheria ya Kulinda Taarifa katika nchi hii ni:
Sheria ya Kulinda Taarifa za Kibinafsi, Official Gazette of the RNM Na. 42 kuanzia 16.02.2022.
Chini ya Sheria hii ya Kulinda Taarifa, Mashahidi wa Yehova wanatumia taarifa za kibinafsi za mhubiri kwa madhumuni ya kidini, kutia ndani mambo yafuatayo:
Chini ya Sheria hii ya Kulinda Taarifa, Mashahidi wa Yehova hutumia taarifa za kibinafsi za wahubiri kwa madhumuni ya kidini, kutia ndani mambo yafuatayo:
kuendeleza na kusimamia dini ya Mashahidi wa Yehova
kushiriki katika mikutano ya kutaniko lolote la Mashahidi wa Yehova na katika utendaji au mradi wowote wa kujitolea
kuamua kushiriki mkutano, kusanyiko la mzunguko, au kusanyiko la eneo lililorekodiwa na kupeperushwa kwa ajili ya kutoa msaada wa kiroho kwa Mashahidi wa Yehova ulimwenguni pote
kushiriki katika mgawo wowote au kutimiza daraka lolote kutanikoni
kudumisha kadi za Rekodi ya Kutaniko ya Mhubiri
kufanyiwa uchungaji na kutunzwa na wazee wa Mashahidi wa Yehova (Matendo 20:28; Yakobo 5:14, 15)
kuweka rekodi ya taarifa za mawasiliano ya dharura ambazo zitatumiwa wakati wa matukio ya dharura.
Taarifa za kibinafsi zitatunzwa kwa muda mrefu kadiri iwezekanavyo kupatana na makusudi yaliyoonyeshwa hapo juu au kwa ajili ya makusudi mengine ya utendaji yanayopatana na sheria. Ikiwa mzazi (au wazazi)/mlezi (au walezi) wa mhubiri ambaye hajafikisha umri wa miaka 18 anaamua kwamba hatatia sahihi fomu ya Makubaliano ya Matumizi ya Taarifa za Kibinafsi (Notice and Consent for Use of Personal Data) baada ya kuombwa kufanya hivyo, Mashahidi wa Yehova hawataweza kutathmini ikiwa mhubiri huyo anastahili kutimiza madaraka fulani katika kutaniko au kushiriki katika utendaji fulani wa kidini.
Mashahidi wa Yehova wanapatikana katika nchi mbalimbali ulimwenguni pote. Kwa sababu hiyo, taarifa za kibinafsi za mhubiri zinaweza kutumwa, kupitishwa, au kuhifadhiwa nje ya nchi aliyopo. Inaweza kutia ndani nchi ambazo sheria za kulinda taarifa ni tofauti kabisa na za nchi ambako habari hizo zilitoka. Mashahidi wa Yehova wanachukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha kwamba habari hizo zinalindwa vizuri. Hatua mojawapo ni kuwa na makubaliano ya kuhamisha taarifa. Watu wanaopokea taarifa hizo ni Mashahidi wa Yehova, nao wanatumia taarifa za kibinafsi za wahubiri kulingana na Sera ya Mashahidi wa Yehova ya Kulinda Habari Ulimwenguni Pote.
Wahubiri wana haki ya kupata taarifa zao: kuomba zisahihishwe, zifutwe, au kuzuia matumizi ya taarifa hizo wanazotuma kwa Mashahidi wa Yehova. Ikiwa wahubiri wametoa idhini taarifa zao zitumiwe kwa ajili ya utendaji mbalimbali, wanaweza kubatilisha wakati wowote makubaliano hayo kuhusiana na matumizi fulani ya wakati ujao ya taarifa zao za kibinafsi. Ikiwa mhubiri atavunja makubaliano kuhusu matumizi ya taarifa zake za kibinafsi au ikiwa mhubiri ataomba taarifa zake za kibinafsi zifutwe au kuzuia matumizi ya taarifa hizo, Mashahidi wa Yehova wanaweza kuendelea kutumia baadhi ya taarifa zake kwa msingi wa madhumuni halali ya kidini au kwa msingi mwingine wa kisheria wanaopata kutokana na Sheria za Kulinda Taarifa. Wahubiri wanatambua kwamba wana haki ya kupeleka malalamiko kwa watu wenye mamlaka ya kulinda taarifa nchini kwao.
Mashahidi wa Yehova wanatumia mipangilio na mbinu mbalimbali za ulinzi kulingana na Sheria ya Kulinda Taarifa ili kulinda taarifa za kibinafsi. Wahubiri wanatambua kwamba taarifa zao za kibinafsi zitashughulikiwa na watu wachache tu walioidhinishwa ili kutimiza madhumuni yaliyoelezwa hapo juu.
Ikiwa una maswali yoyote unaweza kuyatuma kwa ofisa anayeshughulika na kulinda taarifa kupitia anwani ifuatayo ya barua pepe:
DataProtectionOfficer.MK@jw.org
Wahubiri wanatambua kwamba utambulisho na taarifa za mawasiliano za wanaodhibiti taarifa katika nchi wanamoishi, wawakilishi wao au ofisa wao anayelinda taarifa, zinaweza kupatikana katika ukurasa wa Mawasiliano ya Kulinda Taarifa kwenye jw.org.
Inawezekana utaratibu wa Mashahidi wa Yehova wa kushughulikia taarifa ukabadilika kadiri wakati unavyopita kutokana na mabadiliko ya utendaji wetu wa kidini, sheria, na teknolojia. Ikiwa itahitajika kubadili ukurasa huu wa Matumizi ya Taarifa za Kibinafsi, tutaweka mabadiliko hayo kwenye ukurasa huu ili wahubiri waweze kujua taarifa tunazokusanya na jinsi tunavyozitumia. Tafadhali chunguza ukurasa huu mara kwa mara ili uone marekebisho yanayofanywa.