Hamia kwenye habari

Matumizi ya Taarifa za Kibinafsi​—Slovenia

Matumizi ya Taarifa za Kibinafsi​—Slovenia

Mtu anapokuwa mhubiri anatambua kwamba shirika la kidini la ulimwenguni pote la Mashahidi wa Yehova—kutia ndani kutaniko lake, ofisi yake ya tawi na mashirika mengine yanayohusiana na Mashahidi wa Yehova yanatumia taarifa zake za kibinafsi kihalali kwa ajili ya utendaji wa kidini. Wahubiri wanatoa taarifa hizo kwa hiari kwenye makutaniko yao kama inavyoelezwa katika kitabu Tengenezo Linalofanya Mapenzi ya Yehova, ili waweze kushiriki katika utendaji wao wa kidini unaohusiana na ibada yao na wategemezwe kiroho.—1 Petro 5:2.

Wahubiri wanaweza kutoa taarifa za ziada za kibinafsi kwenye tengenezo wanapotaka kujihusisha na shughuli nyingine za kidini. Taarifa za kibinafsi zinatia ndani jina, tarehe ya kuzaliwa, jinsia, tarehe ya kubatizwa, taarifa za mawasiliano, au taarifa zinazohusiana na hali ya kiroho, utendaji wa kazi ya kuhubiri, au daraka lolote ambalo mtu anatimiza katika tengenezo la Mashahidi wa Yehova. Taarifa hizo zinatia ndani habari ambazo zinaonyesha imani ya kidini ya mhubiri na pia zinaweza kutia ndani taarifa nyingine za siri za kibinafsi. Matumizi ya taarifa za kibinafsi yanaweza kumaanisha kukusanya, kurekodi, kupanga, kuunda, na kuhifadhi taarifa hizo, pamoja na njia nyingine yoyote inayofanana na hizo ya kutumia taarifa hizo.

Sheria ya Kulinda Taarifa katika nchi hii ni:

General Data Protection Regulation (EU) 2016/679.

Chini ya Sheria hii ya Kulinda Taarifa, wahubiri wanakubali taarifa zao za kibinafsi zitumiwe na Mashahidi wa Yehova kwa madhumuni ya kidini, kutia ndani mambo yafuatayo:

  • kushiriki katika mikutano ya kutaniko la kwao la Mashahidi wa Yehova na kufanya utendaji au mradi wowote wa kujitolea;

  • kuamua kushiriki mkutano, kusanyiko la mzunguko, au kusanyiko la eneo lililorekodiwa na kurushwa kwa ajili ya kutoa mwongozo wa kiroho kwa Mashahidi wa Yehova ulimwenguni pote;

  • kushiriki kwenye mgawo wowote au kutimiza daraka lolote kutanikoni, ambalo linatia ndani kuangalia jina la mhubiri na mgawo aliopangiwa ambao hubandikwa kwenye ubao wa matangazo katika Jumba la Ufalme la Mashahidi wa Yehova;

  • kudumisha kadi za Rekodi ya Kutaniko ya Mhubiri;

  • kufanyiwa uchungaji na kutunzwa na wazee wa Mashahidi wa Yehova (Matendo 20:28; Yakobo 5:14, 15);

  • kuweka rekodi ya taarifa ya mawasiliano ya dharura ambayo yatatumiwa wakati wa matukio ya dharura.

Taarifa za kibinafsi zitatunzwa kwa muda mrefu kadiri iwezekanavyo kulingana na makusudi yaliyoonyeshwa hapo juu au kwa ajili ya makusudi mengine ya utendaji yanayopatana na sheria. Ikiwa Mhubiri akiamua kutotia sahihi fomu ya Makubaliano ya Matumizi ya Taarifa za Kibinafsi (Notice and Consent for Use of Personal Data), Mashahidi wa Yehova watashindwa kujua ikiwa mhubiri huyo anastahili kutimiza madaraka fulani katika kutaniko au kushiriki katika utendaji fulani wa kidini.

Taarifa za kibinafsi zinaweza kutumwa kwenye shirika lingine la kidini la Mashahidi wa Yehova ikiwa zinahitajika na inafaa kufanya hivyo. Wahubiri wanapaswa kufahamu kwamba baadhi ya mashirika ya kidini yapo kwenye nchi ambako uwiano wa sheria za kulinda taarifa ni tofauti kabisa na nchi yenu. Hata hivyo, wahubiri wanafahamu kwamba wale wote wanaopokea taarifa zao za kibinafsi kutia ndani shirika la kidini lililoko kwenye makao makuu ya Mashahidi wa Yehova kule Marekani, watatumia taarifa hizo za kibinafsi kulingana na Sera ya Mashahidi wa Yehova ya Kulinda Habari Ulimwenguni pote.

Wahubiri wana haki ya kuingia, kuomba taarifa za kibinafsi wanazotuma kwa Mashahidi wa Yehova zifutwe, au kuzuia zisishughulikiwe, na kurekebisha makosa yoyote katika taarifa hizo. Wahubiri wanaweza kubatilisha wakati wowote makubaliano kuhusiana na matumizi fulani ya wakati ujao ya taarifa zao za kibinafsi. Ikiwa mhubiri atavunja makubaliano kuhusu matumizi ya taarifa zake za kibinafsi, Mashahidi wa Yehova wana haki ya kuendelea kutumia baadhi ya taarifa zake za kibinafsi bila makubaliano kama hayo, taarifa hizo zinahusiana na madhumuni ya kidini ya kudumisha na kusimamia taarifa za washiriki za Mashahidi wa Yehova ulimwenguni pote au kwa msingi mwingine wa kisheria ambao wanapata kutokana na Sheria za Kulinda Taarifa. Wahubiri wanatambua kwamba wana haki ya kupeleka malalamiko kwa wenye mamlaka ya kulinda taarifa wa nchini kwao.

Mashahidi wa Yehova wanatumia mipangilio na mbinu mbalimbali za ulinzi kulingana na Sheria ya Kulinda Taarifa ili kulinda taarifa za kibinafsi. Wahubiri wanatambua kwamba taarifa zao za kibinafsi zitashughulikiwa na watu wachache tu walioidhinishwa ili kutimiza madhumuni yaliyoelezwa hapo juu.

Ikiwa una maswali yoyote unaweza kuyatuma kwa ofisa anayeshughulika na kulinda taarifa kupitia anwani ifuatayo ya barua pepe: DataProtectionOfficer.SI@jw.org.

Wahubiri wanajua kwamba utambulisho na taarifa za mawasiliano ya anayedhibiti taarifa katika nchi wanamoishi, na kama inakubalika, mawasiliano ya mwakilishi wake, na ofisa anayeshughulikia masuala ya kulinda taarifa, zinaweza kupatikana katika ukurasa wa Mawasiliano ya Kulinda Taarifa wa jw.org.

Inawezekana utaratibu wa kushughulikia taarifa unaweza kubadilika kulingana na wakati kutokana na mabadiliko ya utendaji wetu wa kidini, sheria, na teknolojia. Ikiwa itafaa kubadili ukurasa huu wa Matumizi ya Taarifa za Kibinafsi, tutatuma mabadiliko hayo kwenye ukurasa huu ili wahubiri waweze kujua taarifa tunazokusanya na jinsi tunavyozitumia. Tafadhali chunguza ukurasa huu mara kwa mara ili uone marekebisho yanayofanywa.