WIMBO 75
Miye Huyu! Unitume!
-
1. Watu wako nachafua
Kabisa jina ya Mungu.
Na wengine wanasema
Ya kama “hakuna Mungu.”
Nani atamutetea
Na kumuimbia sifa?
(REFREE 1)
Miye huyu, unitume!
Nitakuimbia sifa.
Kwangu ni pendeleo sana
Kufanya kazi yako.
-
2. Leo watu wanasema
Yehova anakawia,
Tena hawamuogope;
Wanaabudu sanamu.
Ni nani atawaonya
Kuhusu vita ya Mungu?
(REFREE 2)
Miye huyu, unitume!
Nitawaonya wabaya.
Kwangu ni pendeleo sana
Kufanya kazi yako.
-
3. Wapole wako nalia
Kwa sababu ya mabaya.
Wako natafuta kweli
Yenye kuleta amani.
Nani atawafariji?
Nani atawafundisha?
(REFREE 3)
Miye huyu, unitume!
Nitafundisha wapole.
Kwangu ni pendeleo sana
Kufanya kazi yako.