A7-A
Matukio Muhimu Katika Maisha ya Yesu Duniani—Matukio Yaliyotangulia Huduma ya Yesu
Vitabu Vinne vya Injili Kulingana na Mfuatano wa Matukio
Chati zifuatazo zina ramani zinazoonyesha safari za kuhubiri za Yesu. Mishale kwenye ramani haionyeshi njia hususa aliyofuata badala yake inaonyesha alikoelekea.
Matukio Yaliyotangulia Huduma ya Yesu
WAKATI |
MAHALI |
TUKIO |
MATHAYO |
MARKO |
LUKA |
YOHANA |
---|---|---|---|---|---|---|
3 K.W.K. |
||||||
Yerusalemu, hekalu |
Malaika Gabrieli amtangazia Zekaria kuhusu kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji |
|||||
Karibu 2 K.W.K. |
Nazareti; Yudea |
Malaika Gabrieli amtangazia Maria kuhusu kuzaliwa kwa Yesu; Maria amtembelea Elisabeti mtu wake wa ukoo |
||||
2 K.W.K. |
Eneo lenye milima la Yudea |
Yohana Mbatizaji azaliwa na kupewa jina; Zekaria atabiri; Yohana ataishi jangwani |
||||
2 K.W.K., karibu Okt. 1 |
Bethlehemu |
Yesu azaliwa; “Neno akawa mwili” |
||||
Karibu na Bethlehemu; Bethlehemu |
Malaika awatangazia wachungaji habari njema; malaika wamsifu Mungu; wachungaji wamtembelea mtoto Yesu |
|||||
Bethlehemu; Yerusalemu |
Yesu atahiriwa (siku ya 8); wazazi wake wampeleka hekaluni (baada ya siku 40) |
|||||
1 K.W.K. au 1 W.K. |
Yerusalemu; Bethlehemu; Misri; Nazareti |
Wanajimu wamtembelea; familia inakimbilia Misri; Herode awaua wavulana wadogo; familia yarudi kutoka Misri na waishi Nazareti |
||||
12 W.K., Pasaka |
Yerusalemu |
Yesu mwenye umri wa miaka 12 akiwa hekaluni awauliza walimu maswali |
||||
Nazareti |
Arudi Nazareti; aendelea kuwatii wazazi wake; ajifunza useremala; Maria apata watoto wa kiume wanne, na pia watoto wa kike (Mt 13:55, 56; Mk 6:3) |
|||||
29 W.K., majira ya kuchipua |
Nyikani, Mto Yordani |
Yohana Mbatizaji aanza huduma yake |