SWALI LA 11
Ni Nini Hutokea Mtu Anapokufa?
“Roho yake hutoka, naye hurudi ardhini; siku hiyohiyo mawazo yake hupotea.”
“Walio hai wanajua kwamba watakufa, lakini waliokufa hawajui jambo lolote kamwe . . . Jambo lolote unalofanya kwa mkono wako, lifanye kwa nguvu zako zote, kwa sababu hakuna kazi wala mipango wala ujuzi wala hekima Kaburini, mahali unapokwenda.”
“[Yesu] akawaambia: ‘Rafiki yetu Lazaro amelala usingizi, lakini ninasafiri kwenda huko ili kumwamsha.’ Hata hivyo, Yesu alikuwa akizungumza kuhusu kifo cha Lazaro. Lakini walifikiri anasema kuhusu kupumzika katika usingizi. Ndipo Yesu akawaambia waziwazi: ‘Lazaro amekufa.’”