Kitabu cha Kwanza cha Mambo ya Nyakati 8:1-40

  • Wazao wa Benjamini (1-40)

    • Wazao wa Sauli (33-40)

8  Benjamini+ alimzaa Bela+ mzaliwa wake wa kwanza, wa pili Ashbeli,+ wa tatu Ahara,  wa nne Noha, na wa tano Rafa.  Wana wa Bela walikuwa Adari, Gera,+ Abihudi,  Abishua, Naamani, Ahoa,  Gera, Shefufani, na Huramu.  Hawa walikuwa wana wa Ehudi, viongozi wa koo* za wakaaji wa Geba,+ waliopelekwa uhamishoni kule Manahathi:  Naamani, Ahiya, na Gera—ndiye aliyewapeleka uhamishoni, naye alimzaa Uza na Ahihudi.  Shaharaimu aliwazaa watoto katika eneo* la Moabu baada ya kuwafukuza Wamoabu. Wake zake walikuwa Hushimu na Baara.*  Na kupitia Hodeshi mke wake, alimzaa Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu, 10  Yeuzi, Sakia, na Mirma. Hao walikuwa wanawe, viongozi wa koo.* 11  Na kupitia Hushimu alimzaa Abitubu na Elpaali. 12  Na wana wa Elpaali walikuwa Eberi, Mishamu, Shemedi (aliyejenga Ono+ na Lodi+ pamoja na miji yake), 13  Beria, na Shema. Hao walikuwa viongozi wa koo* za wakaaji wa Aiyaloni.+ Hao ndio waliowafukuza wakaaji wa Gathi. 14  Na kulikuwa na Ahio, Shashaki, Yeremothi, 15  Zebadia, Aradi, Ederi, 16  Mikaeli, Ishpa, Yoha, wana wa Beria; 17  na Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi, 18  Ishmerai, Izlia, Yobabu, wana wa Elpaali; 19  na Yakimu, Zikri, Zabdi, 20  Elienai, Zilethai, Elieli, 21  Adaya, Beraya, Shimrathi, wana wa Shimei; 22  na Ishpani, Eberi, Elieli, 23  Abdoni, Zikri, Hanani, 24  Hanania, Elamu, Anthothiya, 25  Ifdeya, Penueli, wana wa Shashaki; 26  na Shamsherai, Sheharia, Athalia, 27  Yaareshia, Eliya, Zikri, wana wa Yerohamu. 28  Hao walikuwa viongozi wa koo* zao kulingana na wazao wao. Viongozi hao waliishi Yerusalemu. 29  Yeieli, baba ya Gibeoni, aliishi Gibeoni.+ Mke wake aliitwa Maaka.+ 30  Na mwana wake mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, kisha Suri, Kishi, Baali, Nadabu, 31  Gedori, Ahio, na Zekeri. 32  Miklothi alimzaa Shimea. Na wote waliishi karibu na ndugu zao kule Yerusalemu, pamoja na ndugu zao wengine. 33  Neri+ alimzaa Kishi; Kishi akamzaa Sauli;+ Sauli akamzaa Yonathani,+ Malki-shua,+ Abinadabu,+ na Eshbaali.*+ 34  Na mwana wa Yonathani aliitwa Merib-baali.*+ Merib-baali akamzaa Mika.+ 35  Na wana wa Mika walikuwa Pithoni, Meleki, Tarea, na Ahazi. 36  Ahazi akamzaa Yehoada; Yehoada akamzaa Alemethi, Azmavethi, na Zimri. Zimri akamzaa Mosa. 37  Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Rafa, Rafa akamzaa Eleasa, Eleasa akamzaa Aseli. 38  Aseli alikuwa na wana sita, na haya ndiyo majina yao: Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia, na Hanani. Hao wote ndio waliokuwa wana wa Aseli. 39  Na wana wa Esheki ndugu yake walikuwa Ulamu mzaliwa wake wa kwanza, wa pili Yeushi, na wa tatu Elifeleti. 40  Na wana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kushika* upinde, nao walikuwa na wana wengi na wajukuu wengi, jumla yao 150. Hao wote walikuwa wazao wa Benjamini.

Maelezo ya Chini

Yaani, ukoo wa upande wa baba.
Tnn., “shamba.”
Au labda, “baada ya kuwafukuza wake zake Hushimu na Baara.”
Yaani, ukoo wa upande wa baba.
Yaani, ukoo wa upande wa baba.
Yaani, ukoo wa upande wa baba.
Pia aliitwa Ish-boshethi.
Pia aliitwa Mefiboshethi.
Tnn., “kukanyaga.”