Kitabu cha Kwanza cha Samweli 22:1-23

  • Daudi akiwa Adulamu na Mispe (1-5)

  • Sauli aagiza makuhani wa Nobu wauawe (6-19)

  • Abiathari atoroka (20-23)

22  Basi Daudi akaondoka huko+ na kukimbilia katika pango la Adulamu.+ Ndugu zake na nyumba yote ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakashuka na kumfuata huko.  Na watu wote waliokuwa na shida na madeni na malalamishi* wakakusanyika kwake, akawa kiongozi wao. Watu 400 hivi walikuwa pamoja naye.  Baadaye Daudi akaondoka huko na kwenda Mispe kule Moabu na kumwambia hivi mfalme wa Moabu:+ “Tafadhali mruhusu baba yangu na mama yangu wakae pamoja nawe mpaka nitakapojua Mungu atanifanyia nini.”  Basi akawaacha wakae na mfalme wa Moabu, nao wakakaa naye muda wote ambao Daudi alikuwa ndani ya ngome.+  Baada ya muda nabii Gadi+ akamwambia Daudi: “Usikae ndani ya ngome. Ondoka humo uende katika nchi ya Yuda.”+ Kwa hiyo Daudi akaondoka na kwenda katika msitu wa Herethi.  Sauli akasikia kwamba Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wameonekana. Wakati huo Sauli alikuwa ameketi kwenye kilima chini ya mti wa mwesheli kule Gibea+ akiwa ameshika mkuki wake mkononi, na watumishi wake wote walikuwa wamemzunguka.  Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake waliokuwa wamemzunguka: “Tafadhali sikilizeni, enyi Wabenjamini. Je, mwana wa Yese+ atawapa ninyi nyote pia mashamba na mashamba ya mizabibu? Je, atawaweka nyote kuwa wakuu wa maelfu na wakuu wa mamia?+  Ninyi nyote mmepanga njama dhidi yangu! Hakuna yeyote aliyenijulisha wakati mwana wangu mwenyewe alipofanya agano na mwana wa Yese!+ Hakuna yeyote kati yenu anayenihurumia na kunijulisha kwamba mwanangu mwenyewe amemchochea mtumishi wangu mwenyewe dhidi yangu ili anivizie, kama hali ilivyo sasa.”  Kisha Doegi+ Mwedomu, aliyekuwa hapo akiwa msimamizi wa watumishi wa Sauli, akamjibu hivi:+ “Nilimwona mwana wa Yese akija Nobu kwa Ahimeleki mwana wa Ahitubu.+ 10  Naye akamwombea Daudi mwongozo kutoka kwa Yehova na kumpa vyakula. Hata alimpa upanga wa Goliathi yule Mfilisti.”+ 11  Mara moja mfalme akaagiza Ahimeleki mwana wa kuhani Ahitubu na makuhani wote wa nyumba ya baba yake waliokuwa Nobu waitwe. Basi wote wakaja kwa mfalme. 12  Sasa Sauli akasema: “Sikiliza, tafadhali, wewe mwana wa Ahitubu!” naye akajibu: “Naam, bwana wangu.” 13  Sauli akamwambia: “Kwa nini mmepanga njama dhidi yangu, wewe na mwana wa Yese, kwa kumpa mikate na upanga na kumtafutia mwongozo kutoka kwa Mungu? Yeye hunipinga na kunivizia, kama anavyofanya sasa.” 14  Ndipo Ahimeleki akamjibu hivi mfalme: “Ni nani kati ya watumishi wako wote anayeaminika* kama Daudi?+ Yeye ni mkwe wako+ mfalme na mkuu wa walinzi wako na anaheshimika katika nyumba yako.+ 15  Je, unafikiri kwamba leo ndio mara ya kwanza kwangu kumtafutia mwongozo kutoka kwa Mungu?+ Jambo unalosema, ni jambo nisiloweza kamwe kuwazia! Nakusihi mfalme usinikasirikie mimi mtumishi wako na nyumba yote ya baba yangu, kwa maana mimi mtumishi wako sikujua lolote kati ya mambo haya.”+ 16  Lakini mfalme akasema: “Hakika utakufa+ Ahimeleki, wewe pamoja na nyumba yote ya baba yako.”+ 17  Ndipo mfalme akawaambia walinzi* waliomzunguka: “Geukeni na kuwaua makuhani wa Yehova, kwa sababu wamemuunga mkono Daudi! Walijua kwamba ametoroka, lakini hawakunijulisha!” Lakini watumishi hao wa mfalme hawakutaka kuinua mikono yao wawashambulie makuhani wa Yehova. 18  Basi mfalme akamwambia Doegi:+ “Wewe geuka uwashambulie makuhani!” Mara moja Doegi Mwedomu+ akageuka na kuwashambulia hao makuhani yeye mwenyewe. Siku hiyo aliwaua wanaume 85 waliovaa efodi ya kitani.+ 19  Pia, akalishambulia kwa upanga jiji la Nobu,+ jiji la makuhani; aliwaua kwa upanga wanaume na wanawake, watoto wadogo na wale wanaonyonya, ng’ombe dume, punda, na kondoo. 20  Hata hivyo, mwana mmoja wa Ahimeleki mwana wa Ahitubu, aliyeitwa Abiathari,+ akatoroka, akakimbia kumfuata Daudi. 21  Abiathari akamwambia hivi Daudi: “Sauli amewaua makuhani wa Yehova.” 22  Ndipo Daudi akamwambia Abiathari: “Siku ile,+ Doegi Mwedomu alipokuwa huko, nilijua kwa hakika kwamba atamwambia Sauli. Mimi binafsi ninawajibika kwa sababu ya kifo cha kila mtu* katika nyumba ya baba yako. 23  Kaa pamoja nami. Usiogope, kwa kuwa yeyote anayetafuta uhai wako* anatafuta uhai wangu;* nitakulinda.”+

Maelezo ya Chini

Au “waliokuwa na uchungu nafsini.”
Au “aliye mwaminifu.”
Tnn., “wakimbiaji.”
Au “kila nafsi.”
Au “nafsi yako.”
Au “nafsi yangu.”