Ayubu 20:1-29

  • Sofari azungumza kwa mara ya pili (1-29)

    • Adai kwamba Ayubu amemtukana (2, 3)

    • Adai kwamba Ayubu ni mwovu (5)

    • Adai kwamba Ayubu anafurahia dhambi (12, 13)

20  Sofari+ Mnaamathi akajibu:   “Ndiyo sababu mawazo yangu mwenyewe yanayonifadhaisha yananichochea kujibuKwa sababu ya mahangaiko niliyo nayo.   Nimesikia karipio linalonivunjia heshima;Na uelewaji wangu unanichochea* kujibu.   Bila shaka unajua jambo hili tangu zamani,Kwa maana imekuwa hivyo tangu mtu* alipoumbwa duniani,+   Kwamba kelele za shangwe za mwovu ni za muda mfupiNa kushangilia kwa mtu anayemkataa Mungu* ni kwa kipindi kifupi.+   Ingawa ukuu wake hupanda mpaka mbinguniNa kichwa chake hufika mawinguni,   Ataangamia milele kama kinyesi chake mwenyewe;Wale waliozoea kumwona watauliza, ‘Yuko wapi?’   Atatoweka kama ndoto, nao hawatampata;Atafukuzwa mbali kama maono ya usiku.   Jicho lililomwona halitamwona tena,Na mahali pake hapatamwona tena.+ 10  Watoto wake mwenyewe watawaomba maskini msaada,Na mikono yake mwenyewe itarudisha mali aliyochukua.+ 11  Mifupa yake ilijaa nguvu za ujana,Lakini nguvu hizo zitalala pamoja naye mavumbini. 12  Ikiwa uovu ni mtamu kinywani mwake,Ikiwa anauficha chini ya ulimi wake, 13  Ikiwa anauonja na hautemiLakini anauacha ukae kinywani mwake, 14  Chakula chake kitageuka na kuwa kichungu ndani yake;Kitakuwa kama sumu* ya swila ndani yake. 15  Amemeza mali, lakini ataitapika;Mungu ataitoa yote tumboni mwake. 16  Atanyonya sumu ya swila;Meno ya nyoka kipiri yatamuua.* 17  Hataona kamwe vijito vya maji,Mafuriko ya asali na siagi. 18  Atarudisha mali zake bila kuzitumia;* Hatafurahia utajiri wa biashara yake.+ 19  Kwa maana amewaponda na kuwaacha maskini;Amenyakua nyumba ambayo hakujenga. 20  Lakini hatakuwa na amani ndani yake;Mali zake hazitamsaidia kuokoka. 21  Hakuna chochote kinachobaki cha kunyafua;Ndiyo sababu ufanisi wake hautadumu. 22  Mali zake zitakapofikia kilele, mahangaiko yatamkumba;Misiba itamshambulia kwa nguvu zote. 23  Atakapokuwa akijaza tumbo lake,Mungu atammwagia hasira yake kali,Itamnyeshea mpaka ndani ya matumbo yake. 24  Atakapokimbia silaha za chuma,Mishale kutoka katika upinde wa shaba itamchoma. 25  Huchomoa mshale mgongoni mwake,Silaha inayong’aa kutoka kwenye nyongo yake,Naye hushikwa na hofu.+ 26  Giza zito linasubiri hazina zake;Moto ambao haukuwashwa na yeyote utamla;Msiba unamsubiri yeyote atakayeokoka katika hema lake. 27  Mbingu zitafunua kosa lake;Dunia itainuka dhidi yake. 28  Mafuriko yataifagilia mbali nyumba yake;Yatakuwa mafuriko yenye nguvu katika siku ya hasira ya Mungu. 29  Hilo ndilo fungu ambalo Mungu atampa mwovu,Urithi ambao Mungu amemtangazia.”

Maelezo ya Chini

Tnn., “roho inayotoka katika uelewaji wangu inanichochea.”
Au “mwanadamu; Adamu.”
Au “mwasi imani.”
Au “nyongo.”
Tnn., “Ulimi wa nyoka kipiri utamuua.”
Tnn., “naye hatameza.”