Ayubu 28:1-28

  • Ayubu aonyesha tofauti iliyopo kati ya hazina za dunia na hekima (1-28)

    • Jitihada za wanadamu za kuchimba madini (1-11)

    • Hekima ina thamani kuliko lulu (18)

    • Kumwogopa Yehova ndiyo hekima ya kweli (28)

28  “Kuna mahali pa kuchimba fedhaNa mahali pa dhahabu wanayosafisha;+   Chuma hutolewa ardhini,Na shaba huyeyushwa* kutoka katika miamba.+   Mwanadamu hulishinda giza;Huchunguza kwa kina katika utusitusi na giza,Akitafuta mawe yenye madini.   Huzamisha bomba mbali na makao ya watu,Mahali paliposahauliwa, mbali na mahali ambapo watu wanatembea;Wanaume fulani hushuka wakining’inia kwa kamba.   Chakula hukua juu ardhini;Lakini chini, kuna msukosuko kama wa moto.*   Katika mawe hayo kuna yakuti,Na vumbi lake lina dhahabu.   Hakuna ndege awindaye anayejua njia ya kufika huko;Jicho la mwewe mweusi halijaiona.   Hakuna mnyama yeyote wa mwituni mwenye fahari aliyeikanyaga;Mwanasimba hajazunguka huko.   Mwanadamu hugonga mwamba mgumu kwa mkono wake;Huipindua milima kwenye misingi yake. 10  Huchimba mitaro ya maji+ kwenye mwamba;Macho yake huona kila kitu chenye thamani. 11  Huziba chemchemi za mitoNa kufichua vitu vilivyofichwa. 12  Lakini hekima—inaweza kupatikana wapi,+Na kiko wapi chanzo cha uelewaji?+ 13  Hakuna mwanadamu anayetambua thamani yake,+Nayo haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai. 14  Vilindi vya maji vinasema, ‘Haimo ndani yangu!’ Nayo bahari inasema, ‘Haiko pamoja nami!’+ 15  Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi;Wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha.+ 16  Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri+Wala kwa madini ya shohamu na yakuti yasiyopatikana kwa urahisi. 17  Dhahabu na kioo haviwezi kulinganishwa nayo;Wala haiwezi kubadilishwa kwa chombo cha dhahabu bora.*+ 18  Marijani na fuwele hazistahili kutajwa,+Kwa maana mfuko uliojaa hekima una thamani kuliko mfuko uliojaa lulu. 19  Topazi+ ya Kushi haiwezi kulinganishwa nayo;Haiwezi kununuliwa hata kwa dhahabu safi. 20  Lakini hekima hutoka wapi,Na kiko wapi chanzo cha uelewaji?+ 21  Imefichwa kutoka machoni pa kila kiumbe aliye hai+Na kufichwa kutoka kwa ndege wa angani. 22  Maangamizi na kifo husema,‘Masikio yetu yamesikia tu habari zake.’ 23  Mungu anaelewa njia ya kuipata;Yeye peke yake ndiye anayejua inakokaa,+ 24  Kwa maana yeye hutazama mpaka kwenye miisho ya dunia,Naye huona kila kitu chini ya mbingu.+ 25  Alipoupa upepo nguvu*+Na kuyapima maji,+ 26  Alipoiwekea mvua sheria+Na njia kwa ajili ya mawingu ya dhoruba yenye ngurumo,+ 27  Kisha akaiona hekima na kuifafanua;Aliiimarisha na kuijaribu. 28  Naye akamwambia mwanadamu: ‘Tazama! Kumwogopa Yehova—hiyo ndiyo hekima,+Na kuepuka uovu ni uelewaji.’”+

Maelezo ya Chini

Tnn., “humwagwa.”
Inaonekana kwamba maneno haya yanahusu uchimbaji wa madini.
Au “iliyosafishwa.”
Tnn., “uzito.”