Ayubu 41:1-34

  • Mungu aeleza kuhusu Lewiathani anayestaajabisha (1-34)

41  “Je, unaweza kumvua Lewiathani*+ kwa ndoanoAu kuufunga chini ulimi wake kwa kamba?   Je, unaweza kupitisha kamba* kwenye mianzi ya pua yake Au kutoboa mataya yake kwa kulabu?*   Je, atakusihi sana umhurumie,Au je, atazungumza nawe kwa upole?   Je, atafanya agano pamoja nawe,Ili umfanye awe mtumwa wako milele?   Je, utamchezea kama ndegeAu kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako?   Je, wafanyabiashara watamtumia kubadilishana bidhaa? Je, watamgawanya miongoni mwao?   Je, utaijaza ngozi yake mikuki+ Au kichwa chake mikuki ya kuvulia samaki?   Mguse kwa mkono wako;Utakumbuka vita hivyo na kamwe hutarudia kufanya hivyo!   Ni kazi bure kujaribu kumtiisha. Ukimwona tu utashtuka.* 10  Hakuna anayethubutu kumchokoza. Basi ni nani anayeweza kukabiliana nami?+ 11  Ni nani aliyenipa kitu chochote kwanza ili nimlipe?+ Chochote kilicho chini ya mbingu ni changu.+ 12  Sitakaa kimya kuhusu miguu yake,Kuhusu nguvu zake na mwili wake wenye umbo zuri. 13  Ni nani aliyemvua vazi lake la nje? Ni nani atakayeingia katikati ya mataya yake yaliyo wazi? 14  Ni nani anayeweza kuifungua kwa nguvu milango ya kinywa chake?* Meno yake kuzunguka kinywa chote yanatisha. 15  Mgongo wake una safu za magamba*Yaliyoshikamana kabisa pamoja. 16  Kila gamba limeshikamana kabisa na lingineHivi kwamba hewa haiwezi kupenya katikati ya magamba hayo. 17  Yamefungamana pamoja;Yameshikamana na hayawezi kutenganishwa. 18  Mkoromo wake hufanya nuru imweke,Na macho yake ni kama miale ya mapambazuko. 19  Mimweko ya radi hutoka kinywani mwake;Cheche za moto huruka nje. 20  Moshi hufuka kutoka katika mianzi ya pua yake,Kama tanuru linalowaka moto wa matete. 21  Pumzi yake huwasha makaa ya mawe,Na mwali wa moto huruka kutoka kinywani mwake. 22  Shingo yake ina nguvu nyingi,Wanaokutana naye hukimbia kwa hofu. 23  Mikunjo ya ngozi yake imeunganishwa kabisa pamoja;Ni imara, kana kwamba imetengenezwa kwa chuma, nayo haiwezi kutikisika. 24  Moyo wake ni mgumu kama jiwe,Naam, ni mgumu kama jiwe la chini la kusagia. 25  Anapoinuka, hata mashujaa huogopa;Mshindo wake huwababaisha. 26  Hakuna upanga unaomfikia unaoweza kushinda;Wala mkuki, mshale, au ncha ya mshale.+ 27  Yeye huona chuma kama nyasi,Shaba kama ubao uliooza. 28  Mshale haumfanyi akimbie;Mawe ya kombeo huwa kama nyasi kavu kwenye mwili wake. 29  Yeye huona rungu kuwa kama nyasi kavu,Naye huucheka mvumo wa mkuki. 30  Chini, yeye ni kama vigae vyenye ncha kali;Hujinyoosha kwenye matope kama kifaa cha kupuria.+ 31  Hufanya vilindi vichemke kama chungu;Huikoroga bahari kama chungu cha manukato. 32  Anapopita huacha njia ikimetameta. Mtu anaweza kudhani kwamba vilindi vina mvi. 33  Hakuna chochote kilicho kama yeye duniani,Kiumbe aliyeumbwa asiogope. 34  Hukodolea macho chochote chenye kiburi. Yeye ni mfalme wa wanyama wote wa mwituni wenye fahari.”

Maelezo ya Chini

Labda ni mamba.
Tnn., “unyasi.”
Tnn., “mwiba.”
Au “utaanguka chini.”
Tnn., “uso wake.”
Au labda, “Anajivunia safu zake za magamba.”