Ezekieli 41:1-26

  • Patakatifu pa hekalu (1-4)

  • Ukuta na vyumba vya kando (5-11)

  • Jengo la magharibi (12)

  • Majengo yapimwa (13-15a)

  • Sehemu ya ndani ya patakatifu (15b-26)

41  Kisha akanileta kwenye sehemu ya nje ya patakatifu,* naye akapima nguzo za pembeni; zilikuwa na upana wa mikono sita* upande mmoja na mikono sita upande mwingine.  Mlango ulikuwa na upana wa mikono kumi, na kuta za pembeni za mlango zilikuwa mikono mitano upande mmoja na mikono mitano upande wa pili. Akapima urefu wake, ambao ulikuwa mikono 40, na upana wake, mikono 20.  Kisha akaingia ndani* na kupima nguzo ya pembeni ya mlango, nayo ilikuwa na unene wa mikono miwili, na mlango ulikuwa na upana wa mikono sita. Kuta za pembeni za mlango zilikuwa* mikono saba.  Kisha akapima chumba kilichotazamana na sehemu ya nje ya patakatifu, na urefu wake ulikuwa mikono 20, na upana wake mikono 20.+ Naye akaniambia: “Hapa ndipo Patakatifu Zaidi.”+  Kisha akapima ukuta wa hekalu, na unene wake ulikuwa mikono sita. Na vyumba vya kando kuzunguka hekalu vilikuwa na upana wa mikono minne.+  Vyumba vya kando vilikuwa na ghorofa tatu, moja juu ya nyingine, na kila ghorofa ilikuwa na vyumba 30. Kulikuwa na vidato kuzunguka pande zote za ukuta wa hekalu ambavyo vilishikilia vyumba vya kando, ili vishikio visiguse ukuta wa hekalu lenyewe.+  Pande zote mbili za hekalu zilikuwa na njia iliyopindapinda* ambayo ilipanuka kadiri ilivyopanda kuelekea vyumba vya juu.+ Upana uliongezeka kutoka ghorofa moja hadi nyingine kadiri mtu alivyopanda kutoka ghorofa ya chini hadi ya juu akipitia ghorofa ya katikati.  Nikaona kwamba kulikuwa na jukwaa lililoinuliwa kuzunguka hekalu, na misingi ya vyumba vya kando ilikuwa na urefu wa utete mmoja wa mikono sita mpaka kwenye pembe.  Upana wa ukuta wa nje wa vyumba vya kando ulikuwa mikono mitano. Kulikuwa na eneo lililo wazi* kando ya vyumba vya kando vilivyokuwa sehemu ya hekalu. 10  Kati ya hekalu na vile vyumba vya kulia chakula*+ kulikuwa na eneo lenye upana wa mikono 20 kila upande. 11  Kulikuwa na mlango kati ya vyumba vya kando na eneo lililo wazi lililokuwa upande wa kaskazini na mlango mwingine upande wa kusini. Upana wa eneo lililo wazi ulikuwa mikono mitano pande zote. 12  Jengo lililokuwa magharibi likitazama eneo lililo wazi lilikuwa na upana wa mikono 70 na urefu wa mikono 90; ukuta wa jengo hilo ulikuwa na unene wa mikono mitano pande zote. 13  Akapima hekalu, nalo lilikuwa na urefu wa mikono 100. Lile eneo lililo wazi, jengo,* na kuta zake zilikuwa pia na urefu wa mikono 100. 14  Upana wa upande wa mbele wa hekalu uliotazama mashariki na pia wa eneo lililo wazi ulikuwa mikono 100. 15  Akapima urefu wa jengo lililotazama eneo lililo wazi upande wa nyuma, pamoja na mabaraza yake pande zote mbili, na urefu wake ulikuwa mikono 100. Pia akapima sehemu ya nje ya patakatifu, sehemu ya ndani ya patakatifu,+ na zile kumbi za ua, 16  pia vizingiti, madirisha yenye viunzi ambavyo ukubwa wake ulipungua kutoka nje kwenda ndani,+ na mabaraza yaliyokuwa katika sehemu hizo tatu. Karibu na kizingiti kulikuwa na mbao+ zilizofunika kuta kuanzia sakafuni mpaka kwenye madirisha; nayo madirisha yalikuwa yamefunikwa. 17  Pia alipima sehemu ya juu ya mlango na sehemu ya ndani ya hekalu na nje na kuzunguka ukuta wote. 18  Kulikuwa na michongo ya makerubi+ na pia michongo ya mitende,+ kila mtende ulikuwa kati ya makerubi wawili, na kila kerubi alikuwa na nyuso mbili. 19  Uso wa mwanadamu ulitazama mtende upande mmoja, na uso wa simba* ulitazama mtende upande wa pili.+ Ilichongwa hivyo katika hekalu lote. 20  Kuanzia sakafuni mpaka sehemu iliyo juu ya mlango kulikuwa na michongo ya makerubi na michongo ya mitende kwenye ukuta wa patakatifu. 21  Miimo ya milango* ya patakatifu ilikuwa mraba.+ Mbele ya mahali patakatifu* kulikuwa na kitu kama 22  madhabahu ya mbao+ iliyokuwa na kimo cha mikono mitatu, na urefu wa mikono miwili. Ilikuwa na nguzo za pembeni, na sehemu yake ya chini* na kuta zake zilitengenezwa kwa mbao. Kisha akaniambia: “Hii ndiyo meza iliyo mbele za Yehova.”+ 23  Kulikuwa na milango miwili katika sehemu ya nje ya patakatifu na pia mahali patakatifu.+ 24  Milango ilikuwa na bawaba mbili zilizozunguka, bawaba mbili kwa kila mlango. 25  Kulikuwa na michongo ya makerubi na michongo ya mitende kwenye milango ya patakatifu, kama ile iliyokuwa ukutani.+ Pia kulikuwa na kifuniko* cha mbao juu ya upande wa mbele wa ukumbi kwa nje. 26  Pia kulikuwa na madirisha yenye viunzi ambavyo ukubwa wake ulipungua kutoka nje kwenda ndani+ na michongo ya mitende pande zote mbili za ukumbi, pia kwenye vyumba vya kando vya hekalu na vifuniko.

Maelezo ya Chini

Tnn., “hekalu.” Katika sura ya 41 na 42, neno hili linamaanisha sehemu ya nje ya mahali patakatifu (Patakatifu) au sehemu yote ya mahali patakatifu (hekalu kutia ndani Patakatifu na Patakatifu Zaidi).
Hiki ni kipimo cha mikono mirefu. Angalia Nyongeza B14.
Yaani, kwenye sehemu ya ndani ya mahali patakatifu, au Patakatifu Zaidi.
Tnn., “upana wa mlango ulikuwa.”
Inaonekana inarejelea ngazi za duara.
Inaonekana ni njia nyembamba iliyozunguka hekalu.
Au “vile vyumba.”
Yaani, jengo la upande wa magharibi wa mahali patakatifu.
Au “mwanasimba mwenye manyoya marefu shingoni.”
Tnn., “Mwimo wa mlango.” Inaonekana maneno haya yanarejelea njia ya kuingia Patakatifu.
Inaonekana inarejelea Patakatifu Zaidi.
Tnn., “urefu wake.”
Au “paa dogo.”