Mwanzo 5:1-32

  • Kuanzia Adamu mpaka Noa (1-32)

    • Adamu azaa wana na mabinti (4)

    • Enoko alitembea na Mungu (21-24)

5  Hiki ndicho kitabu cha historia ya Adamu. Siku ambayo Mungu alimuumba Adamu, alimuumba kwa mfano wa Mungu.+  Mwanamume na mwanamke aliwaumba.+ Siku ambayo aliwaumba,+ aliwabariki na kuwaita Binadamu.*  Adamu aliishi miaka 130, kisha akazaa mwana kwa mfano wake, kwa sura yake, akampa jina Sethi.+  Baada ya kumzaa Sethi, Adamu aliishi miaka 800. Naye akazaa wana na mabinti.  Basi siku zote za maisha ya Adamu zilikuwa miaka 930, kisha akafa.+  Sethi aliishi miaka 105, akamzaa Enoshi.+  Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807. Naye akazaa wana na mabinti.  Basi siku zote za maisha ya Sethi zilikuwa miaka 912, kisha akafa.  Enoshi aliishi miaka 90, kisha akamzaa Kenani. 10  Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815. Naye akazaa wana na mabinti. 11  Basi siku zote za maisha ya Enoshi zilikuwa miaka 905, kisha akafa. 12  Kenani aliishi miaka 70, kisha akamzaa Mahalaleli.+ 13  Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840. Naye akazaa wana na mabinti. 14  Basi siku zote za maisha ya Kenani zilikuwa miaka 910, kisha akafa. 15  Mahalaleli aliishi miaka 65, kisha akamzaa Yaredi.+ 16  Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830. Naye akazaa wana na mabinti. 17  Basi siku zote za maisha ya Mahalaleli zilikuwa miaka 895, kisha akafa. 18  Yaredi aliishi miaka 162, kisha akamzaa Enoko.+ 19  Baada ya kumzaa Enoko, Yaredi aliishi miaka 800. Naye akazaa wana na mabinti. 20  Basi siku zote za maisha ya Yaredi zilikuwa miaka 962, kisha akafa. 21  Enoko aliishi miaka 65, kisha akamzaa Methusela.+ 22  Baada ya kumzaa Methusela, Enoko aliendelea kutembea na Mungu wa kweli kwa miaka 300. Naye akazaa wana na mabinti. 23  Basi siku zote za maisha ya Enoko zilikuwa miaka 365. 24  Enoko aliendelea kutembea na Mungu wa kweli.+ Kisha hakuwepo tena, kwa maana Mungu alimchukua.+ 25  Methusela aliishi miaka 187, kisha akamzaa Lameki.+ 26  Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782. Naye akazaa wana na mabinti. 27  Basi siku zote za maisha ya Methusela zilikuwa miaka 969, kisha akafa. 28  Lameki aliishi miaka 182, kisha akazaa mwana. 29  Akamwita mwana huyo Noa,*+ akisema: “Huyu atatufariji katika kazi yetu ngumu na katika kazi inayoumiza ya mikono yetu kwa sababu ya ardhi iliyolaaniwa+ na Yehova.” 30  Baada ya kumzaa Noa, Lameki aliishi miaka 595. Naye akazaa wana na mabinti. 31  Basi siku zote za maisha ya Lameki zilikuwa miaka 777, kisha akafa. 32  Baada ya Noa kuishi miaka 500, alimzaa Shemu,+ Hamu,+ na Yafethi.+

Maelezo ya Chini

Au “Adamu; Wanadamu.”
Huenda jina hili linamaanisha “Pumziko; Faraja.”