Yoshua 16:1-10

  • Urithi wa wazao wa Yosefu (1-4)

  • Urithi wa kabila la Efraimu (5-10)

16  Na nchi ambayo wazao wa Yosefu+ waligawiwa*+ ilianzia Yordani huko Yeriko hadi kwenye vijito vilivyo upande wa mashariki wa Yeriko, na kupitia nyikani hadi Yeriko katika eneo lenye milima la Betheli.+  Ilianzia Betheli ambayo ni sehemu ya Luzi na kuendelea hadi kwenye mpaka wa Waarki huko Atarothi,  nayo ikashuka kwenda magharibi hadi kwenye mpaka wa Wayafleti kufikia mpaka wa Beth-horoni+ ya Chini na Gezeri,+ na kufika kwenye bahari.  Na wazao wa Yosefu,+ yaani, watu wa kabila la Manase na kabila la Efraimu, wakamiliki nchi yao.+  Na huu ndio mpaka wa wazao wa Efraimu kulingana na koo zao: Mpaka wa urithi wao upande wa mashariki ulikuwa Ataroth-adari,+ hadi Beth-horoni ya Juu,+  na mpaka huo ulifika kwenye bahari. Mikmethathi+ ilikuwa upande wa kaskazini, na mpaka huo ulizunguka upande wa mashariki hadi Taanath-shilo, kuelekea upande wa mashariki hadi Yanoa.  Kisha ukashuka kutoka Yanoa hadi Atarothi na Naara na kupita Yeriko+ hadi Yordani.  Kutoka Tapua+ ukaelekea magharibi hadi kwenye Bonde la Kana, na kufika kwenye bahari.+ Huo ndio urithi wa kabila la Efraimu kulingana na koo zao;  na wazao wa Efraimu walikuwa pia na majiji yaliyozungukwa katikati ya urithi wa wazao wa Manase.+ 10  Lakini hawakuwafukuza Wakanaani waliokuwa wakikaa Gezeri,+ na tangu wakati huo Wakanaani wanaishi miongoni mwa wazao wa Efraimu+ wakifanya kazi za kulazimishwa.+

Maelezo ya Chini

Au “waligawiwa kwa kura.”