WIMBO NA. 111 Sababu za Kuwa na Shangwe Chagua Rekodi ya Sauti Sababu za Kuwa na Shangwe Samahani, programu ya kupakia faili hiyo imeshindwa kupakia. Pakua Video Hii Onyesha Kama Maandishi Ficha Aina ya Maandishi (Mathayo 5:12) 1. Tuna sababu nyingi sana, Kuwa na shangwe halisi. Watu wa mataifa yote, Wanajiunga na sisi. Tunashangilia moyoni, Neno linaeleweka. Tunajifunza kila siku; Imani yaongezeka. Nayo shangwe yetu yazidi, Kama moto uwakao. Ingawa tuna matatizo, Kwetu Yehova ni ngao. (KORASI) Yehova ni shangwe yetu, Kazi zake za ajabu. Mawazo yake yapita yetu, Mungu mwema na mkuu! 2. Tunaziona kazi zake, Mbingu, bahari, dunia. Anastahili kusifiwa, Kwa kazi za uumbaji. Sasa twatangaza ushindi, Wa Ufalme wa Yehova. Ujumbe wa baraka zake, Kotekote twatangaza. Siku mpya yakaribia, Sikuzote kuwe shangwe. Dunia nazo mbingu mpya, Milele tushangilie. (KORASI) Yehova ni shangwe yetu, Kazi zake za ajabu. Mawazo yake yapita yetu, Mungu mwema na mkuu! (Ona pia Kum. 16:15; Isa. 12:6; Yoh. 15:11.) Inayotangulia Inayofuata Chapa Shiriki Shiriki Sababu za Kuwa na Shangwe ‘MWIMBIENI YEHOVA KWA SHANGWE’ Sababu za kuwa na shangwe (Wimbo Na. 111) Lugha ya Alama ya Tanzania Sababu za kuwa na shangwe (Wimbo Na. 111) https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/1102016911/sign/wpub/1102016911_sign_sqr_xl.jpg sjj 111