WIMBO NA. 18

Tunathamini Fidia

Tunathamini Fidia

(Luka 22:20)

  1. 1. Twasimama mbele

    za kiti cha enzi,

    Yah ulituonyesha

    Upendo mkubwa.

    Ulitoa Mwana wako

    wa pekee.

    Ni zawadi kubwa sana,

    twaithamini.

    (KORASI)

    Alimwaga damu yake.

    Tupate kuwekwa huru.

    Twashukuru,

    kwa moyo wetu wote milele.

  2. 2. Kwa hiari Yesu

    Katoa dhabihu.

    Na kwa upendo katoa

    Uhai wake.

    Kafungua njia

    Tupate wokovu.

    Sasa tumaini la

    uzima tunalo.

    (KORASI)

    Alimwaga damu yake.

    Tupate kuwekwa huru.

    Twashukuru,

    kwa moyo wetu wote milele.