WIMBO NA. 24 Njooni Kwenye Mlima wa Yehova Chagua Rekodi ya Sauti Njooni Kwenye Mlima wa Yehova Samahani, programu ya kupakia faili hiyo imeshindwa kupakia. Pakua Video Hii Onyesha Kama Maandishi Ficha Aina ya Maandishi (Isaya 2:2-4) 1. Tazama uone, Mlima wa Yehova. Uko, juu zaidi, Kuliko mingine. Toka pande zote, Watu wamiminika. Nao waita wengi, Wamwabudu Mungu. Mdogo, mnyonge, Atakuwa taifa kubwa. Twapiga hatua, Yehova anatubariki. Umati mkubwa, Unajiunga nasi. Nao waukubali Ufalme wa Mungu. 2. Agizo tunalo, La kuhubiri Neno. Nasi tunatangazia wote Ufalme. Kristo atawala, Awahimiza wote. Kote duniani Wamsikie Yeye. Neno la Yehova, Linawafungulia njia. Tunayo furaha, Kuwasaidia wengine! Sote tushiriki Kwa kuwasaidia Watu wajue Mungu Wapate uzima. (Ona pia Zab. 43:3; 99:9; Isa. 60:22; Mdo. 16:5.) Inayotangulia Inayofuata Chapa Shiriki Shiriki Njooni Kwenye Mlima wa Yehova ‘MWIMBIENI YEHOVA KWA SHANGWE’ Njooni Kwenye Mlima wa Yehova (Wimbo Na. 24) Lugha ya Alama ya Tanzania Njooni Kwenye Mlima wa Yehova (Wimbo Na. 24) https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/1102016824/sign/wpub/1102016824_sign_sqr_xl.jpg sjj 24