WIMBO NA. 58

Kutafuta Marafiki wa Amani

Kutafuta Marafiki wa Amani

(Luka 10:6)

  1. 1. Yesu kaweka kielelezo,

    Kwa kutangaza Ufalme,

    Popote alipokuwa.

    Aliwapenda kondoo wote.

    Siku nzima hakuchoka

    hadi usiku.

    Milangoni na njiani,

    Tunazo habari njema,

    U karibu mwisho wa matatizo.

    (KORASI)

    Twatafuta

    Kote rafiki wa amani.

    Twatafuta

    Moyo utakao wokovu.

    Twahubiri

    Kotekote.

  2. 2. Hatuna muda wa kupoteza.

    Mamilioni ya watu,

    Wako hatarini leo.

    Upendo wetu hutuchochea.

    Kufariji watu wote,

    Na kuwafunza.

    Vijijini na mijini,

    Astahilipo mmoja,

    Kwa pamoja sote twashangilia.

    (KORASI)

    Twatafuta

    Kote rafiki wa amani.

    Twatafuta

    Moyo utakao wokovu.

    Twahubiri

    Kotekote.