WIMBO NA. 61

Songeni Mbele, Enyi Mashahidi!

Songeni Mbele, Enyi Mashahidi!

(Luka 16:16)

  1. 1. Watu wa Mungu wameazimia,

    Kazi ya kuhubiri itatimia.

    Shetani akiwavamia,

    Kwa nguvu za Mungu wavumilia.

    (KORASI)

    Haya tusonge mbele Ee Mashahidi!

    Kufanya kazi ya Mungu na tuzidi!

    Yaja Paradiso aliyoahidi,

    Yehova Mungu tumhimidi.

  2. 2. Askari wa Yehova wanakesha.

    Ulimwengu hautawatetemesha.

    Na uovu wajiepusha.

    Utimilifu wetu twadumisha.

    (KORASI)

    Haya tusonge mbele Ee Mashahidi!

    Kufanya kazi ya Mungu na tuzidi!

    Yaja Paradiso aliyoahidi,

    Yehova Mungu tumhimidi.

  3. 3. Enzi ya Mungu yadharauliwa.

    Jina lake kuu limechafuliwa.

    Karibuni litatakaswa.

    Mbele za wote litatambulishwa.

    (KORASI)

    Haya tusonge mbele Ee Mashahidi!

    Kufanya kazi ya Mungu na tuzidi!

    Yaja Paradiso aliyoahidi,

    Yehova Mungu tumhimidi.