WIMBO NA. 95

Nuru Inazidi Kuongezeka

Nuru Inazidi Kuongezeka

(Methali 4:18)

  1. 1. Kale manabii walitabiri

    Kristo tumaini la wote.

    Roho ya Yehova ilifunua,

    Masihi angewakomboa.

    Sasa Kristo Yesu anatawala

    Ishara zinaonyesha.

    Tuna pendeleo kujua hayo,

    Malaika huchungulia!

    (KORASI)

    Nuru inazidi kung’aa;

    Twatembea kwenye nuru.

    Yehova atufunulia;

    Aongoza njia zetu.

  2. 2. Yesu ametupa mtumwa wake,

    Anayetulisha kiroho.

    Na nuru ya kweli yaongezeka

    Inatuchochea mioyo.

    Njia yetu yaonekana wazi

    Twatembea kwenye nuru.

    Asante Yehova! Chanzo cha kweli,

    Asante kwa kutuongoza.

    (KORASI)

    Nuru inazidi kung’aa;

    Twatembea kwenye nuru.

    Yehova atufunulia;

    Aongoza njia zetu.