WIMBO NA. 97

Uhai Unategemea Neno la Mungu

Uhai Unategemea Neno la Mungu

(Mathayo 4:4)

  1. 1. Neno la Yehova Mungu,

    Hututegemeza.

    Hatuishi kwa mkate,

    Bali Neno Lake.

    Latupa amani, shangwe,

    na baraka nyingi.

    (KORASI)

    Hatuishi kwa Mkate;

    Bali Neno Lake.

    Latupa tuhitajiyo;

    Latutegemeza.

  2. 2. Neno linasimulia,

    Watu wa zamani.

    Wenye imani thabiti.

    Washikamanifu.

    Tusomapo kuwahusu,

    Tunatiwa moyo.

    (KORASI)

    Hatuishi kwa Mkate;

    Bali Neno Lake.

    Latupa tuhitajiyo;

    Latutegemeza.

  3. 3. Tusomapo Neno Lake,

    Twapata faraja.

    Matatizo yazukapo,

    Latupa hekima.

    Tuthamini tusomayo,

    Na tusikiayo.

    (KORASI)

    Hatuishi kwa Mkate;

    Bali Neno Lake.

    Latupa tuhitajiyo;

    Latutegemeza.