SEHEMU YA 5

Gharika Kubwa​​—Nani Alimsikiliza Mungu? Nani Hakumsikiliza?

Gharika Kubwa​​—Nani Alimsikiliza Mungu? Nani Hakumsikiliza?

Watu wengi katika siku za Noa walitenda mabaya. Mwanzo 6:5

Adamu na Hawa walipata watoto, na watu wakawa wengi duniani. Baada ya muda, malaika fulani walijiunga na Shetani katika uasi wake.

Wakaja duniani na wakajifanyia miili ya kibinadamu ili waweze kuoa wanawake. Wanawake hao wakazaa wana wenye kutisha na wenye nguvu waliokuwa na uwezo unaopita wa wanadamu.

Ulimwengu ukajaa watu waliofanya mambo mabaya. Biblia inasema: “Uovu wa mwanadamu ulikuwa mkubwa duniani na kwamba kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake ulikuwa mbaya tu wakati wote.”

Noa alimsikiliza Mungu na akajenga safina. Mwanzo 6:13, 14, 18, 19, 22

Noa alikuwa mtu mzuri. Yehova alimwambia Noa kwamba angewaharibu watu waovu kwa gharika kubwa.

Pia, Mungu akamwambia Noa ajenge meli kubwa, inayoitwa safina, na aingize humo familia yake pamoja na wanyama wa kila aina.

Noa aliwaonya watu kuhusu Gharika iliyokuwa inakaribia, lakini hawakumsikiliza. Baadhi yao walimcheka; wengine wakamchukia.

Safina ilipokamilika, Noa aliwaingiza wanyama ndani.