WIMBO NA. 112

Yehova, Mungu wa Amani

Yehova, Mungu wa Amani

(Wafilipi 4:9)

  1. 1. Mungu wa upendo,

    Yehova Mungu wetu,

    Twakuomba roho yako,

    Tukuze sifa zako.

    Ulitununua,

    Kwa damu ya Mwanao.

    Twaomba utukubali

    Tupe amani Yako.

  2. 2. Roho yako wewe,

    Yatupa ufahamu.

    Twaongozwa na kulindwa

    Katika ulimwengu.

    Tunatazamia

    Mwisho wa matatizo.

    Tupe roho takatifu,

    Tuishi kwa amani.

  3. 3. Umewakusanya

    Wale uwapendao.

    Tumependelewa sana,

    Kukuabudu wewe.

    Utawala wako,

    Utaleta baraka.

    Kisha watumishi wako,

    Waishi kwa amani.