WIMBO NA. 114 “Iweni na Subira” Chagua Rekodi ya Sauti “Iweni na Subira” Samahani, programu ya kupakia faili hiyo imeshindwa kupakia. Pakua Video Hii Onyesha Kama Maandishi Ficha Aina ya Maandishi (Yakobo 5:8) 1. Yehova, Baba yetu, Anapenda jina lake. Ataka litakaswe, Lawama liondolewe. Kavumilia mengi, Tena muda mrefu; Ana subira nyingi, Hajachoka kamwe. Ataka watu wote Wapate kuokolewa. Aonyesha subira, Kwa faida yetu sote. 2. Nasi tunahitaji, Kuionyesha subira. Ghadhabu tuepuke. Tukae kwa utulivu. Tuzingatie mema, Wafanyayo wengine. Tutumaini mema, Japo matatizo. Na sifa za Kikristo, Tuonyeshe sikuzote. Na kwa kufanya hivyo, Tumuige Mungu wetu. (Ona pia Kut. 34:14; Isa. 40:28; 1 Kor. 13:4, 7; 1 Tim. 2:4.) Inayotangulia Inayofuata Chapa Shiriki Shiriki “Iweni na Subira” ‘MWIMBIENI YEHOVA KWA SHANGWE’ “Iweni na Subira” (Wimbo Na. 114) Lugha ya Alama ya Tanzania “Iweni na Subira” (Wimbo Na. 114) https://cms-imgp.jw-cdn.org/img/p/1102016914/sign/wpub/1102016914_sign_sqr_xl.jpg sjj 114