WIMBO NA. 85

Karibishaneni

Karibishaneni

(Waroma 15:7)

  1. 1. Mwakaribishwa mikutanoni.

    Mjifunze Neno la Mungu.

    Linalotupa sote uhai;

    Tunauthamini mwaliko wa Mungu.

  2. 2. Asante Mungu, kwa wachungaji,

    Ndugu zetu watupendao.

    Twawathamini, twawaheshimu

    Na wengine pia twawakaribisha.

  3. 3. Enyi wanyo’fu, mwakaribishwa,

    Kuipata njia ya kweli.

    Mungu na Kristo, wametuvuta.

    Tukaribishane kwa moyo mweupe.